Ushahidi mpya waihusisha kampuni ya Apple na mzozo wa madini, wanasheria wa DRC wasema

Ushahidi mpya waihusisha kampuni ya Apple na mzozo wa madini, wanasheria wa DRC wasema

Wanasheria hao wameiataka kampuni hiyo kujibu tuhuma za mnyonyoro wake ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Madini mengi yanayopatikana nchini humo hutumika katika uzalishaji wa vifaa vya kielektroniki./Picha: Reuters

Wanasheria wa kimataifa wanaoiwakilisha serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku ya Jumatano ushahidi mpya uliokusanywa kutoka kwa watoa taarifa unaoonesha kwamba Apple inachimba madini kutoka katika maeneo yenye migogoro mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yao, mawakili hao waliitaka Apple kujibu tuhuma kuhusu ugavi wake nchini humo, na walisema walikuwa wanatathmini hatua za kisheria za kuchukua.

Hata hivyo, kampuni ya Apple haikujibu tuhuma hizo kwa Reuters.

Mawakili wa Congo walimjulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook mnamo Aprili 22 juu ya ugavi wake, na pia waliandikia kampuni tanzu za Apple nchini Ufaransa, wakitaka majibu ndani ya wiki tatu.

Wanasheria kutoka Amsterdam & Partners LLP walisema katika taarifa yao Jumatano kwamba, wiki nne baadaye, "mtu mkuu wa teknolojia amekaa kimya na hakujibu au hata kukiri kupokea maswali.

"Tumepokea ushahidi mpya. Ni wakati muafaka kwa kampuni ya Apple kutoa majibu kuhusu maswali haya," alisema Robert Amsterdam, mmoja ya mawakili hao.

TRT Afrika
Reuters