Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amekosoa vikali chapisho la hivi majuzi la Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz akimlenga Rais wa Türkiye Recep Tayyip Erdogan. / Picha: Jalada la AA

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki, Fahrettin Altun, amekemea ujumbe wa hivi karibuni wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli, Israel Katz, linalomlenga Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akisema, "Uturuki haina chochote cha kujifunza kutoka kwa wauaji wenye kiu ya damu na mauaji ya kimbari."

"Hakuna chochote Rais wetu au nchi yetu inaweza kujifunza kutoka kwa wauaji wenye kiu ya damu na mauaji ya kimbari kama nyinyi! Mauaji mliyofanya dhidi ya ndugu zetu Wapalestina, pamoja na mauaji ya kimbari ya aibu mliyotekeleza, siku moja mtawajibika," Altun alisema katika taarifa kwenye X siku ya Ijumaa.

"Kadri unavyotamka jina la Recep Tayyip Erdogan kwa mdomo wako mchafu, unaotoa damu ya wasio na hatia, ndivyo tutakavyomuunga mkono na kusimama naye kwa uthabiti zaidi."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, pia alikemea ujumbe wa Katz kwenye mitandao ya kijamii linalomlenga Erdogan, akiliita "ugonjwa".

"Tabia ya Katz ya kila mara kulenga nchi yetu na Rais wetu mpendwa kwa hisia zake za kufikirika, badala ya kutimiza majukumu yake kama Waziri wa Mambo ya Nje, ni ugonjwa wa hali ya juu," Fidan alisema kwenye ukurasa wake wa X.

"Mtu huyu, ambaye uwepo wake katika baraza la mawaziri umetengwa tu kwa kutoa matusi na uongo, ni sanamu ya upuuzi na ujasiri wa serikali ya kikatili ya Netanyahu," Fidan aliongeza.

TRT World