Israel imewaacha takriban watu 600,000 huko Gaza bila maji safi na salama/ Picha: AFP

Uholanzi imewataka raia kuondoka Lebanon

Uholanzi imetoa ushauri kwa raia wake na kuwataka kuondoka nchini Lebanon "haraka iwezekanavyo" kutokana na mvutano unaoendelea katika eneo hilo.

Wizara ya Mambo ya Nje siku ya Ijumaa ilitoa tahadhari kuhusu X, ikiwataka raia wa Uholanzi kuepuka kusafiri kwenda Lebanon na wale wanaoishi huko kuondoka "haraka iwezekanavyo" wakati bado safari za ndege za kibiashara zikiendelea kuwepo.

Wizara pia iliwataka raia wa Uholanzi walioamua kubaki nchini Lebanon kuendelea kuwasiliana na ubalozi wa Beirut na kuwa tayari kwa dharura yoyote itakayotokea.

Watu 600,000 huko Gaza wamenyimwa maji safi na salama

Israel imewaacha takriban watu 600,000 huko Gaza bila maji safi na salama baada ya kukata huduma hiyo kuanzia tarehe Oktoba 11, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu (HRW) limesema, likitahadharisha kuongezeka kwa janga la kibinadamu linaloongezeka katika eneo lililozingirwa la Palestina.

Israel inasema sasa iko tayari kuheshimu ombi la rais wa Marekani Joe Biden la kuruhusu msaada mdogo wa kibinadamu kuingia Gaza/ Picha:AA

"Kuzingirwa kwa Gaza kunawaweka watoto wa Kipalestina na raia wengine katika hatari kubwa," HRW ilisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

"Chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, mataifa lazima yaheshimu haki ya maji, ambayo ni pamoja na kujiepusha na kuzuia upatikanaji au kuharibu huduma za maji na miundombinu kama "hatua ya adhabu" wakati wa migogoro ya silaha," imesema HRW.

Israel yakubali kuruhusu msaada kuingia Gaza

Israel inasema sasa iko tayari kuheshimu ombi la rais wa Marekani Joe Biden la kuruhusu msaada mdogo wa kibinadamu kuingia Gaza.

Rais Joe Biden anasema alifikia makubaliano na mwenzake wa Misri kuruhusu msururu wa kwanza wa magari 20 yaliyokuwa yamebeba misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, mpaka ambao Israel iliufunga baada ya shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7.

Mashirika ya Red Crescent Society ya Misri na Palestina na Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kusaidia kusimamia operesheni hiyo, ili kuhakikisha vifaa kutoka kwa msafara huo kupitia Kivuko cha Rafah kwenye mpaka wa Misri na Gaza vinawafikia walengwa.

Idadi ya majeruhi ya Israeli inaongezeka

Wizara ya Afya ya Israel inasema idadi ya Waisraeli waliojeruhiwa tangu kuanza kwa mzozo wa kivita na kundi la Palestina Hamas mnamo Oktoba 7 imeongezeka hadi 4,834.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara siku ya Ijumaa, watu 12 wako wapo mahututi, huku 280 wako katika hali mbaya, na 771 wakiwa katika hali ya wastani, na wengine wamepata majeraha madogo. Ilibainisha kuwa Waisraeli 301 waliojeruhiwa bado wanatibiwa na kwamba idadi ya vifo imefikia 1,400 tangu Oktoba 7.

Tuzo za Muziki za MTV Europe zimesitishwa kutokana na mzozo

Waandaaji wa Tuzo za Muziki za MTV Ulaya zilizopangwa kufanyika mwezi ujao mjini Paris wanasema kuwa hafla hiyo imesitishwa hadi hapo baadae, kwa sababu ya "kuyumba kwa matukio ya ulimwengu" kutokana na mzozo unaoendelea Israel na Gaza.

"Kutokana na kuyumba kwa matukio ya dunia, tumeamua kutoendelea na MTV EMA 2023 kutokana na tahadhari nyingi kwa maelfu ya wafanyakazi, wasanii, mashabiki na washirika wanaosafiri kutoka pembe zote za dunia kwenda katika maonyesho hayo," msemaji alisema katika taarifa Alhamisi.

Wanajeshi wa Israel wameondoka katika kambi ya wakimbizi

Wanajeshi wa Israel wameondoka katika kambi ya wakimbizi baada ya mashambulizi ya saa 30. Jeshi la Israel liliondoka katika kambi ya wakimbizi ya Nour Shams katika mji wa Tulkarem kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Kambi hii inakaliwa kwa mabavu siku ya Ijumaa asubuhi kufuatia mashambulizi ya saa 30, ambayo Tel Aviv ilieleza kuwa "operesheni ya kijeshi."

Walioshuhudia tukio hilo waliliambia Shirika la Habari la Anadolu kwamba mashambulizi ya Israel dhidi ya kambi hiyo yamesababisha vifo vya Wapalestina 12 na kujeruhi makumi ya wengine.

Wakati wa mashambulizi ya jeshi la Israel, lilishambulia eneo katika kambi hiyo kwa kutumia ndege isiyo na rubani, walioshuhudia pia walisema, na kuongeza kuwa wanajeshi wa Israel walifanya uharibifu mkubwa katika kambi hiyo.

Shambulio la Israeli dhidi ya Kanisa la Orthodox

Watu kadhaa waliuawa katika shambulio la Israeli dhidi ya Kanisa la Orthodox la Ugiriki.

Takriban Wapalestina nane waliuawa katika shambulio la anga la Israel dhidi ya Kanisa la Orthodox la Kigiriki la Saint Porphyrius katika mji wa Gaza, kulingana na shirika la habari la Wafa la Palestina.

TRT Afrika