| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Saif al-Islam Gaddafi, mtota wa aliyekuwa rais wa Libya, ameripotiwa kuuawa
Hakuna maelezo zaidi kuhusu kifo cha Gaddafi hadi sasa.
Saif al-Islam Gaddafi, mtota wa aliyekuwa rais wa Libya, ameripotiwa kuuawa
Seif al-Islam Gaddafi alipohudhuria kikao katika chumba cha mahakama mjini Zintan, Mei 25, 2014. / / Reuters
tokea masaa 6

Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, ameripotiwa kuuawa, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na familia yake, wakili wake Khaled el-Zaydi, pamoja na vyombo vya habari vya Libya, vilitoa taarifa hiyo siku ya Jumanne.

Hadi sasa hakuna maelezo zaidi kuhusu kifo cha Gaddafi.

Ingawa Saif al-Islam alikuwa maarufu nchini humo, hasa kwa nafasi yake katika kuunda sera za serikali kabla ya mwaka 2011, umaarufu wake hadharani umepungua katika miaka ya hivi karibuni.

Mwaka 2015, mahakama ya Libya ilimhukumu adhabu ya kifo licha ya kutokuwepo mahakamani, kwa tuhuma za kukandamiza maandamano ya amani wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyoangusha utawala wa baba yake.

Pia alishtakiwa kwa muda na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, kesi ambayo mawakili wake walishindwa kuifuta.

Mnamo mwaka 2021, Saif al-Islam alijiandikisha kugombea urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Disemba, lakini uchaguzi huo hatimaye ulisambaratika kutokana na mkwamo wa kisiasa.

CHANZO:Reuters