Umoja wa Afrika / Photo: Reuters

By Coletta Wanjohi

Ripoti ya Amnesty International inasema Umoja wa Afrika ulipata mafanikio fulani, hasa katika kuimarisha amani na usalama katika baadhi ya maeneo ya bara hilo.

Uchambuzi huo ulioangazia hali ya haki za binadamu mwaka 2022 duniani ulihusisha nchi 156. Umetoa changamoto kwa Umoja wa Afrika kuwa na maamuzi zaidi katika nchi ambazo raia bado hawajapata afueni kutokana na mizozo.

"Mwaka wa 2022 ulitoa fursa kwa Umoja wa Afrika kusherehekea miaka 20, kuchukua hatua kali za ujasiri katika kushughulikia mizozo ya bara na maswala ya ukiukaji wa haki za binadamu," anasema Japhet Biegon, kiongozi wa kikanda wa shirika la Amnesty International.

Je, ni yapi baadhi ya mambo muhimu ya ripoti hiyo?

Maendeleo yaliyo patikana

Kamati ya Afrika ya wataalamu wa haki na ustawi wa mtoto iligundua kuwa sera ya Tanzania ya kutengwa dhidi ya wasichana wajawazito shuleni ilikiuka mkataba wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto na kupendekeza sera hiyo iangaliwe upya.

Nchini Zimbabwe, sheria inayo haramisha ndoa za utotoni kuanzishwa.

Nchini Sierra Leone, watoto 800, wakiwemo wasichana wajawazito na wasichana ambao walikuwa wameacha shule kwa sababu ya ujauzito walirudishwa tena shuleni.

Sudan Kusini mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye umri wa miaka 15 aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa tarehe 14 Novemba 2017 aliachiliwa.

Vikwazo vya kubadilishwa

Umoja wa Afrika umepewa changamoto ya kufanya maamuzi madhubuti ya kuanzisha mahakama ya mseto nchini Sudan Kusini.

Nchini Ethiopia, AU imeshutumiwa kuwa kimya zaidi huku serikali ya Ethiopia kuendelea kukashifu na kunyima Tume ya Afrika ya Uchunguzi wa Haki za Kibinadamu na Watu kuhusu Hali uwezo wa kuingia katika eneo la Tigray.

Mgogoro wa vita unaendelea Somalia, Ethiopia, Mali, Burkina Faso, DRC na hii bado ni changamoto kwa raia.

Uhaba wa chakula ulizidi kuwa mbaya kutokana na migogoro na ukame katika nchi kadhaa za Afrika na kuwaacha watu wengi wakikabiliwa na njaa kali.

Nchi zilizoathiriwa zikiwemo Angola, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kenya, Madagascar, Niger, Somalia, Sudan Kusini na Sudan.

TRT Afrika