Shambulio la Israeli dhidi ya Iran katika mkoa wa Isfahan. / Picha: AFP

Hakukuwa na shambulio la kombora dhidi ya Iran, afisa mmoja wa Iran ameliambia shirika la habari la Reuters, akipinga ripoti za awali za vyombo vya habari vya Marekani kuhusu shambulio la kombora dhidi ya nchi hiyo.

Msemaji wa shirika la anga za juu la Iran pia amenukuliwa akisema kuwa hakuna ripoti za mashambulizi ya makombora, na ulinzi wa anga wa nchi hiyo ilipiga risasi ndege kadhaa zisizo na rubani angani juu ya mkoa wa Isfahan.

Maafisa wawili wa Marekani hata hivyo wameithibitishia shirika la habari la CBS, kwamba kombora la Israel limeipiga Iran. Shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Israel imeitaarifu Marekani mapema kuhusu mashambulizi hayo.

Makombora ya Israeli

Kulikuwa na ripoti kwamba makombora ya Israeli yameshambulia eneo la Iran, shirika la habari la ABC iliripoti, ikimnukuu afisa wa Marekani.

Shirika la habari la Fars kutoka Iran pia limesema milipuko ilisikika katikati mwa uwanja wa ndege wa Isfahan, lakini sababu haikujulikana.

"Chanzo cha sauti hizi bado hakijajulikana, na uchunguzi unaendelea hadi maelezo kamili ya tukio hilo yatakapobainishwa," shirika la habari la Fars lilisema. Ndege za kibiashara zilianza kubadilisha njia zao asubuhi ya Ijumaa na kuelekea magharibi mwa Iran, shirika la habari la AP liliripoti.

Vita vya Gaza

Wajumbe kutoka Marekani na Israel walikuwa wamefanya mkutano wa kawaida kujadili mvutano unaoongezeka kati ya Tel Aviv na Iran, pamoja na hatua ya kijeshi ya Israeli kuvamia mji wa Rafah kusini mwa Gaza.

Sehemu kubwa ya taarifa ya Ikulu ya Marekani siku ya Alhamisi ililenga Iran, saa chache baada ya msemaji kusema kwamba timu hizo zitajadili kwa kiasi kikubwa Rafah.

Taarifa rasmi ya Ikulu ya Marekani ya mkutano huo ilisema "mkutano ulianza na watu kidogo kujadili shambulio la Iran, na juhudi za pamoja za kuimarisha ulinzi wa Israeli ya kuwa na uwezo wa hali ya juu, na kadhalika ushirikiano wa kijeshi."

Wakati huo huo, Mkuu wa Pentagon Austin pia alizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant siku ya Alhamisi kujadili vitisho vya kikanda na hatua za Iran katika Mashariki ya Kati.

TRT World