Wajumbe 12 wa UNSC walipiga kura kuunga mkono ombi la Palestina, Marekani wamepinga. / Picha: Reuters

Marekani siku ya Alhamisi ilikataa ombi la Wapalestina lililopiganiwa kwa muda la kutaka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, na kupinga hatua ya Baraza la Usalama, licha ya kuongezeka kwa masikitiko ya kimataifa juu ya hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza.

Hatua hiyo ya mshirika mkuu wa Israel ilitarajiwa kabla ya upigaji kura, uliyofanyika zaidi ya miezi sita baada ya mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya Gaza, kulipiza kisasi shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na wapiganaji wa Hamas kusini mwa Israel.

Nchi kumi na mbili zilipiga kura kuunga mkono rasimu ya azimio lililopendekeza uanachama kamili wa Wapalestina. Huku Uingereza na Uswizi kujizuia kupiga kura.

Ofisi ya kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas iliita hatua hiyo ya Marekani kama "uchokozi wa wazi" na "kutia moyo wanaotekeleza vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wetu... ambavyo vinasukuma eneo hilo zaidi hadi kwenye ukingo wa shimo."

'Udhalimu wa kihistoria'

Rasimu ya azimio hilo ilitaka kupendekezwa kwa Baraza Kuu "kwamba nchi ya Palestina ikubaliwe uanachama wa Umoja wa Mataifa" badala ya uanachama usiyokuwa na faida", ambayo imekuwa nayo tangu 2012.

Kabla ya kura hiyo, mjumbe maalum wa Mamlaka ya Palestina Ziad Abu Amr ameliambia Baraza hilo kwamba "kuipa Palestina uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa kutaondoa baadhi ya dhulma za kihistoria ambazo vizazi vinavyofuata vya Palestina vingefanyiwa."

TRT World