| swahili
Maoni
UTURUKI
4 dk kusoma
Vita vya Sudan: Kuiondoa UAE na kuiweka Uturuki kunaweza kuimarisha juhudi za kimataifa za amani
Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua muhimu kuwaokoa wananchi wa Sudan dhidi ya wapiganaji wa RSF na washirika wao wa kigeni.
Vita vya Sudan: Kuiondoa UAE na kuiweka Uturuki kunaweza kuimarisha juhudi za kimataifa za amani
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Abdel Fattah al Burhan, Rais wa Baraza Kuu la Sudan wakiwa katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya. /
17 Novemba 2025

Na Mayada Kamal Eldeen

Kwa sasa, juhudi za kimataifa zinaendelea ili kumaliza mgogoro mkubwa wa kibinadamu unaoendelea Sudan na kusitisha mauaji yanayofanywa na wapiganaji wa RSF dhidi ya raia wa Darfur.

Kutokana na hilo, Marekani, Misri, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE) waliunda kamati ya pamoja kuratibu mahitaji ya dharura ya Sudan.

Wakati RSF wanaendeleza vita vya kikatili vinavyohatarisha uhai na utu nchini Sudan—ikijumuisha uhalifu wa vita uliopangwa katika miji ya Al Fasher na Bar huko Darfur na Kordofan—kuna taarifa za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja nchini Marekani yanayojumuisha nchi nne maarufu “Quartet.”

Kwa hakika, mazungumzo hayo yanapaswa kupingwa kwa kuwa tangu 2022 hayajazaa matunda ya kusitisha vita vinavyoteketeza nchi.

Kwa upande mwingine, Uturuki imekuwa ikiisimamia Sudan kama rafiki na ndugu wa kweli, ikijitahidi mno kumaliza migogoro nchini humo. Kwa sababu hizi, UAE inapaswa kubadilishwa na Uturuki ndani ya mazunumzo yanayojumuisha nchi nne (Quartet) ya kusimamia amani Sudan. Sababu mahsusi za pendekezo hili ni pamoja na:

Uturuki haina upendeleo, na haijawahi kuchukua upande unaofaidisha kundi moja dhidi ya jingine, jambo linaloipa nafasi pana ya mazungumzo yenye kuaminika.

Uturuki ina historia chanya ya mahusiano na Sudan, ambayo inarejea hadi kipindi cha Utawala ya Ottoman, jambo linalojenga msingi wa uaminifu na heshima kati ya mataifa haya mawili.

Rais Recep Tayyip Erdogan anaheshimika sana nchini Sudan, katika jamii, siasa na jeshi.

Erdogan hubainisha umuhimu wa kibinadamu kuliko maslahi ya kisiasa, jambo linalodhihirishwa na misaada ya chakula na matibabu inayotolewa na Uturuki.

Ufanisi wa kidiplomasia wa Uturuki

Uturuki imeonyesha uwezo wa hali ya juu katika upatanishi, hasa Afrika na kanda nzima. Mifano muhimu ni:

1. Kutatua mzozo kati ya Ethiopia na Somalia mnamo 2024, ambapo Uturuki ilimaliza mzozo wa muda mrefu kuhusu upatikanaji wa Ethiopia wa bandari, mzozo uliotishia ustawi wa Pembe ya Afrika kwa miongo kadhaa. 

2. Upatanishi kati ya Urusi na Ukraine, kupitia Mpango wa Usafirishaji Nafaka wa 2022, uliookoa mamilioni ya watu dhidi ya njaa.

3. Upatanishi katika Libya na Syria, ambako Uturuki imekuwa na mchango mzuri katika kutuliza migogoro tata.

4. Mazungumzo ya Somalia na Somaliland (2013–2014) yaliyosababisha kupatikana kwa Mkataba wa Ankara. 

Uzoefu huu unaonesha uwezo wa Uturuki kukabiliana na migogoro yenye sura nyingi. Waziri wa Mambo ya Nje, Hakan Fidan, anatambuliwa kimataifa kama mmoja wa wanadiplomasia hodari zaidi.

 

Mnamo Desemba 12, 2024, Rais Erdogan alitoa pendekezo rasmi kwa Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan wa Sudan, na Sudan ikalikaribisha mara moja.

Baadaye, Januari 5, 2025, Burhanettin Duran— Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki—alisafiri hadi Port Sudan kukutana na viongozi wa juu wa nchi hiyo, ambapo dhamira ya Uturuki katika kuleta amani ilisisitizwa.

Hata UAE ilikubali nafasi ya Uturuki, ishara kuwa wahusika wote wako tayari kukubali msuluhishi huyu.

Hatua madhubuti za Uturuki kwa Sudan

Uturuki haikuishia kwenye ahadi pekee; imechukua hatua za dhati. Ubalozi wake Sudan umeendelea kufanya kazi wakati wa vita, tofauti na mataifa mengi makubwa kama Marekani, Ufaransa na Ujerumani ambayo yaliwaondoa wanadiplomasia wake. Balozi Fatih Yıldız amekuwa pamoja na watu wa Sudan kwa ukaribu na uaminifu.

Uturuki pia ina mtandao mpana wa mahusiano na mataifa muhimu kama Marekani, Umoja wa Ulaya, Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Afrika, pamoja na Urusi na China. Hii inaiwezesha kuwa na nafasi kubwa ya kuhimiza amani Sudan.

Kwa muktadha huu, ni muhimu Uturuki iwe sehemu ya nchi nne (Quartet) ili kusukuma usitishaji haraka wa mapigano na kujenga msingi wa amani ya kudumu.

Ikiwa Uturuku itachukua nafasi ya UAE—ambayo serikali ya Sudan imekuwa ikilaumu kwa kuiunga mkono RSF—hilo litakuwa hatua muhimu kuelekea amani.

Ikiwa Ankara itaongoza mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jeshi la Sudan na RSF, miji ya Ankara au Istanbul inaweza kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo kwa uaminifu na usalama.

Ingawa UAE imekanusha mara kwa mara kuhusika, serikali ya Sudan imetoa madai makali kwamba UAE imetoa silaha kwa wapiganaji wa RSF. Kwa sababu hii UAE inaweza kujaribu kupinga Uturuki ichukue nafasi yake. Walakini, UAE ilikuwa tayari imekubali nafasi ya Uturuki mnamo Desemba 2024.

Baada ya uhalifu wa kivita na mauaji ya kutisha ambayo yalitikisa ulimwengu katika siku tatu baada ya kuanguka kwa Al Fasher, shinikizo la kimataifa linaweza kulazimisha mabadiliko haya.

Aidha, UAE inaweza kupendelea kujiondoa ili kulinda hadhi yake.

Kwa ujumla, chaguo ni wazi. Wakati ni sasa. Jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua hii muhimu ili kuokoa Sudan na watu wake kutoka kwa RSF na washirika wa kigeni.

Mwandishi: Dr. Mayada Kamal Eldeen, Profesa Msaidizi wa Sayansi ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Chuo Kikuu cha Tokat Gaziosmanpaşa, Türkiye.

Maoni ya mwandishi hayaakisi msimamo au sera za TRT Afrika.

 

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Uturuki inakaribisha makubaliano ya amani kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23
Uungwaji mkono wa Ujerumani unaashiria 'upya wa nia ya kisiasa' kwa ombi la Uturuki la EU: Fidan
Fidan: Njia ya kusuluhisha vikwazo vya Marekani iko wazi huku Trump akionyesha nia yake
Rais Erdogan aadhimisha kumbukumbu ya miaka 42 ya kuanzishwa kwa TRNC
Rais Erdogan afungua maonyesho ya 'Echoes' Istanbul kwa heshima ya Sule Yuksel Senler na Malcolm X
Uturuki yaadhimisha miaka 81 ya kupelekwa uhamishoni Waturuki wa Ahiska kutoka Georgia
Hafla yafanyika Uturuki ya kuwakumbuka wanajeshi waliofariki kwenye ajali ya ndege
Wanajeshi 20 wa Uturuki wafariki katika ajali ya ndege ya mizigo ya kijeshi huko Georgia: wizara
Wanajeshi 20 wa Uturuki wauawa katika ajali ya ndege ya shehena ya kijeshi huko Georgia: wizara
Ndege ya kijeshi ya mizigo ya Uturuki yaanguka mpakani mwa Georgia na Azerbaijan ikiwa na watu 20
Uimarishaji wa Uturuki ni heshima na kumuenzi Ataturk: Erdogan
Uturuki inamkumbuka Ataturk miaka 87 baada ya kufariki
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki kuzuru Marekani siku ya Jumatatu
Rais Erdogan anatumai Marekani itatimiza ahadi zake kuhusu makubaliano ya ndege za kivita za F-35
Palestina inapongeza amri za kukamatwa dhidi ya maafisa 37 wa Israel kutoka Uturuki kama 'ushindi
Ujumbe wa Erdogan 'Azerbaijan haiko peke yake' ulipelekea ushindi wa Karabakh: Aliyev
Ushindi wa Karabakh wa Azerbaijan kwa amani ya Caucasus: Rais Erdogan
Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu, juu ya mashtaka ya mauaji
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Uturuki kuandaa mazungumzo ya Gaza wiki ijayo kufuatia wasiwasi juu ya usitishaji mapigano – Fidan