| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya na Uganda kwa pamoja wazindua mradi wa reli ya kisasa-SGR
Mpango wa upanuzi wa reli hadi mpaka wa Uganda ulikuwa umesimama kwa zaidi ya miaka 6 kutokana na matatizo ya kifedha na ufadhili.
Kenya na Uganda kwa pamoja wazindua mradi wa reli ya kisasa-SGR
Upanuzi wa reli kutoka Kisumu hadi Malaba umeanza / Picha: Kenya Railways / Public domain
tokea masaa 11


Rais William wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda kwa pamoja wamezindua upanuzi wa reli utoka mji wa Kisumu nchini Kenya.

Reli hii ya aina ya SGR imepangwa kwenda hadi mji wa Malaba mpakani na Uganda.

"Haikuwa reli ya kupotea ilikuwa ni mpango wetu kwamba SGR hii ya Kisumu hadi Malaba itakuwa reli ya ustawi na mabadiliko ya Kenya," Rais wa Kenya William Ruto alisema katika uzinduzi huo jijini Kisumu.

Mpango wa upanuzi ulikuwa umesimama kwa zaidi ya miaka 6 kutokana na matatizo ya kifedha na ufadhili.

Kwa Uganda isiyo na bandari ambayo inategemea bandari ya Kenya ya Mombasa, reli hiyo itarahisisha usafirishaji wa shehena zake.

"Reli hii ni sehemu ya urekebishaji wa mfumo wetu wa usafiri hasa kwa upande wa Uganda, ambao hauna mantiki na ubadhirifu. Mpango wetu ni kusafirisha mizigo mizito kwa reli,” Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema katika uzinduzi huo.

Katika kipindi cha miaka minane iliyopita, SGR imesafirisha zaidi ya abiria milioni 15 na zaidi ya tani milioni 45 za mizigo.

Sehemu ya kwanza ya reli, inayounganisha bandari ya Mombasa hadi Nairobi, ilikamilika mwaka wa 2017.

Lakini baada ya China kupunguza ufadhili wa miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika, mradi huo ulikwama katika maeneo ya Bonde la Ufa, umbali wa zaidi ya kilomita 350 kutoka mpaka wa Uganda.

Hii sasa iliziba kiungo cha kuvuka mpaka kilichopangwa ili kuongeza uhusiano wa kikanda na biashara.

"Imepunguza gharama ya usafiri, kuboresha ufanisi na kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wetu," Rais Ruto aliongeza.

Kama msingi wa fedha za ujenzi, Kenya sasa inatumia fedha zinazotokana ushuru wa maendeleo ya reli unaotozwa kwa mizigo inayobebwa kwa awalmu hii mpya ya ujenzi wa reli.

Ushuru huu unakadiriwa kuwa takriban dola milioni 270 kila mwaka.

China inasalia kuhusika katika mradi wa upanuzi ikiwa kampuni ya China Road and Bridge Corporation (CRBC) ndiyo mkandarasi mkuu wa awamu hiyo mpya.

Tangu kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Standard Gauge mwaka wa 2014 nchini Kenya shughuli za usafirishaji zimezalisha zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa mwezi huku mapato ya abiria yameongezeka kwa asilimia 40.

CHANZO:TRT Swahili