| swahili
SIASA
1 dk kusoma
Djibouti: Abdoulkader Houssein Omar ateuliwa Waziri mpya wa Mambo ya Nje
Tamko la uteuzi huo lilitiwa saini na Rais Ismail Omar Guelleh, ambaye amekuwa madarakani toka mwaka 1999, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwengine mwaka 2026.
00:00
Djibouti: Abdoulkader Houssein Omar ateuliwa Waziri mpya wa Mambo ya Nje
Tamko ta uteuzi huo, lilitolewa na ofisi ya Rais wa nchi hiyo, siku ya Jumanne./Picha: Wengine
1 Aprili 2025

Serikali ya Djibouti imemteua  Abdoulkader Houssein Omar kama Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya Mahamoud Ali Youssouf, ambaye mwezi Februari mwaka huu, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU).

Tamko ta uteuzi huo, lilitolewa na ofisi ya Rais wa nchi hiyo, siku ya Jumanne.

Omar, ambaye ni balozi wa Djibouti kwenye nchi za Kuwait na Jordan, aliteuliwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, akichukua nafasi ya Youssouf ambaye aliitumikia kwa miaka 20.

"Haya sio mabadiliko ya baraza la mawaziri, ni mabadiliko tu ndani ya serikali," alisema Alexis Mohamed, msemaji wa ofisi ya Rais wa Djibouti katika mahojiano yake na AFP.

Tamko la uteuzi huo lilitiwa saini na Rais Ismail Omar Guelleh, ambaye amekuwa madarakani toka mwaka 1999, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwengine mwaka 2026.

CHANZO:AFP