Simulizi ya maendeleo barani Afrika mara nyingi huelezwa kupitia mitazamo ya kawaida: misaada kutoka nje, mikopo, na mabadiliko ya serikali. Lakini wadau wa maendeleo zaidi ni raia wenye asili ya bara hilo wanaoishi nje ya nchi.
Watu zaidi ya milioni 170 wenye asili ya Afrika ni sehemu ya watu wanaoishi nje ya nchi, licha ya uwezo wao kutozingatiwa vyema.
Tafakari hili. Kulingana na Benki ya Dunia, Kusini mwa Jangwa la Sahara ilipata mapato ya dola bilioni 49 mwaka 2021. Kufikia 2024, wastani unaonesha kuwa idadi iliongezeka maradufu hadi dola bilioni 95 ikiwa zaidi ya misaada inayopokea nchi kadhaa. Misri (bilioni $22.7) na Nigeria (bilioni $19.8) yakiwa mataifa yanayoongoza kupokea fedha kutoka raia wake walioko nchi za nje.
Familia zinategemea fedha hizi kwa ajili ya chakula, ada za shule, matibabu, na kulipa kodi. Matumizi pekee hayawezi kuimarisha uchumi. Kuelekeza sehemu ya fedha hizi katika uwekezaji kungebadilisha pakubwa muelekeo wa maendeleo barani Afrika.
Utafiti wa 2023 kuhusu maendeleo duniani ambapo wataalamu walioko katika mataifa ya nje wanachangia kupitia kazi za muda mfupi, kutoa ushauri, ushirikiano wa mafunzo, na majukumu maalum bila kuhamia katika mataifa husika.
Bara la Afrika halihitaji kuanzisha vitu vipya. Inahitaji kuona raia wake walioko nje siyo kama wageni, bali washirika: wawekezaji, wabunifu, mabalozi wa kitamaduni, na watetezi. Dalili zinaonesha kuwa raia wenye asili ya Afrika walioko nje wako tayari. Swali ni je Afrika iko tayari kuafikiana nao.
Wakati wa kufanya hivyo ni sasa. Kwa kutumia sera sahihi, mifumo ya uwekezaji, na njia za kubadilishana mbinu, raia walioko nje ya nchi wanaweza kuwa chachu ya kubadilisha uchumi na utamaduni wa bara la Afrika. Muamko wa bara la Afrika uko njiani siyo kwa misaada kutoka nje, bali kupitia watu wake.
Mwandishi, Dkt. Sunny Ofehe, Ni Msaidizi Mwandamizi Gavana la Jimbo la Delta nchini Nigeria wa Masuala Ushirikiano wa Nje















