| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Trump atishia 'kusambaratisha' vinu vya nishati vya Iran iwapo haitafunguwa Hormuz
Awali Iran imesema "haitavumilia" iwapo miundombinu yake itashambuliwa.
Trump atishia 'kusambaratisha' vinu vya nishati vya Iran iwapo haitafunguwa Hormuz
Trump atishia kuvishambulia vinu vya nishati vya Iran iwapo haitafungua Mlango Bahari wa Hormuz. / AP
tokea masaa 14

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia "kusambaratisha" vinu vya nishati vya Iran, akianza na vikubwa, iwapo Iran haitafungua Mlango Bahari wa Hormuz ndani ya saa 48.

"Iwapo Iran haitafungua kikamilifu, bila tishio, Mlango Bahari wa Hormuz, ndani ya saa 48 kuanzia sasa, Marekani itashambulia na kusambaratisha vinu vyao vya nishati, ikianza na vikubwa kabisa," alindika katika mtandao wa Truth Social Jumamosi.

Aliandika tishio hilo saa moja na dakika 44 usiku saa za Marekani (2344GMT), akimaanisha mwisho ya tishio lake ni Jumatatu.

Hata hivyo, hakusema hasa ni kinu gani anachomaanisha ni kikubwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema Ijumaa kwamba Iran "haitavumilia" iwapo miundombinu yake itashambuliwa.

Trump awali aliiambia PBS kwamba alijizuia kushambulia vinu vya nishati vilivyopo Tehran kwa sababu athari yake ingekuwa kubwa kwa miaka mingi kwa raia wa nchi hiyo.

Tishio hili linaonesha hali inavyozidi kuwa mbaya.

Mlango Bahari wa Hormuz

Tangu Marekani na Israel kuanzisha mapigano dhidi ya Iran Februari 28, Iran imefunga Mlango Bahari wa Hormuz kama sehemu ya kulipiza kisasi.

Tangu kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz ambao ndio unaotumika kupitisha sehemu kubwa ya mafuta na gesi, kampuni kadhaa za ushafirishaji zimeanza kutumia njia mbadala hivyo kuongeza gharama ya usafirishaji.