Hafsa Abdiwahab Sheikh
Vita vya Sudan vimebadilika kutoka mvutano wa kisiasa na kuwa hali mbaya zaidi kwa watu duniani na janga la kiafya, huku matatizo yakiwa hata nje ya mipaka ya nchi hiyo.
Mzozo huu mbaya katika ya Jeshi la Sudan (SAF) na wapiganaji wa RSF umeharibu miundombinu muhimu, kudhoofisha mifumo ya afya, na mamilioni ya watu kukimbia makazi yao.
Huku njaa ikizidi, hospitali zikishindwa kutoa huduma na watu kukimbia, ni wazi kuwa mzozo huu umekuwa suala la dharura kwa kanda.
Diplomasia inayoongozwa na Afrika, uhakika wa misaada inahitajika mara moja. Umuhimu wa kisiasa unatakiwa ubakie Afrika.
Watu wamepitia madhila makubwa, Kulingana na ripoti ya shirika la UNICEF Sudan (Januari 2025), watu zaidi ya milioni 30 — ikiwa ni nusu ya idadi ya watu wa Sudan -sasa wanahitaji msaada wa dharura, na watu kati ya milioni 12 na milioni 14 wameondoka katika makazi yao, kuifanya Sudan kuwa eneo lenye watu wengi zaidi waliokimbia makazi yao.
Familia zinapata hifadhi katika magofu, majengo ya shule, na kambi za muda, mara nyingi ikiwa hakuna maji safi, mazingira mabaya ya usafi na kutopatikana chakula.
Kila takwimu kuna maisha ambayo yanakatisha tamaa, wazazi wanaoshindwa kuwapa watoto chakula, watoto kukosa elimu, na jamii kunyimwa haki ya kuwa salama.
Njaa ni kali katika maeneo ya Kordofan Kusini na Darfur, huku Al Fasher ikiwa kitovu cha matatizo hayo.
Kulingana na Mendy Hameda, aliyekuwa Balozi wa Amani wa Umoja wa Afrika kwa Afrika Mashariki, ambaye kwa sasa anasimamia juhudi za asasi isiyokuwa ya serikali ya Sudan HRRDS (Hope Relief and Rehabilitation for Disabilities Support), mapigano na mashambulizi yanaendelea ndani na karibu ya mji wa Al Fasher.
Hospitali, zahanati na mabohari yanatakiwa yasiwe uwanja wa vita na yatambuliwe kama maeneo ya kuwapa watu hifadhi.
Njia za kufikisha misaada zainahitaji kufunguliwa tena na kuwa na uangalizi wa uwazi ili kuepuka misaada kupelekwa maeneo yasiyostahili. Miradi ya dharura ya lishe na juhudi za chanjo kwa wingi, hasa kwa watoto zinaonesha dalili za utapiamlo kwa watoto, lazima zipewe kipaumbele.
Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha matatizo makubwa zaidi. Mashirika ya msiaada yanaonya kuhusu familia kushindwa kupata milo kwa zaidi ya siku kadhaa, kusafiri mwendo mrefu kutafuta maji safi, na kuuza wanavyomiliki ili waweze kuishi.
Sudan ikiingia kwenye matatizo zaidi, kutasababisha mzozo mkubwa katika kanda: kufanya watu waingie katika nchi jirani kwa wingi, kudhoofisha usalama mipakani, kuwa na kuhatarisha njia za biashara na hofu kubwa katika Upembe wa Afrika na eneo la Sahel.
Usalama nchini Sudan siyo tu suala tu la kibinadamu — bali ni umuhimu zaidi kimkakati.
Bara la Afrika lazima lichukuwe jukumu la kuongoza, na washirika duniani waunge mkono juhudi—kwa sababu umuhimu wa kisiasa lazima ubakie Afrika.
Mamilioni ya raia wa Sudan wanasubiri uongozi ambao unatambuwa umuhimu wa suala hili na kushughulikia kwa dharura inayohitajika.
Mwandishi, Hafsa Abdiwahab Sheikh ni mwandishi wa kujitegemea na mtafiti anayeangazia siasa za Afrika Mashariki.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.















