| swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumatatu alimteua balozi wa nchi hiyo nchini China, Khamis Mussa Omar, kuwa waziri wa fedha katika baraza lake jipya la mawaziri kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi uliopita.
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitangaza Baraza jipya la Mawaziri, jijini Dodoma, tarehe 17 Novemba, 2025. @ikulu_Tanzania
17 Novemba 2025

Katika hotuba yake ya moja kwa moja, Rais Samia amesema Anthony Mavunde ataendela kuwa waziri wa madini na Mahmoud Thabit Kombo kuendelea kuwa waziri wa mambo ya nje.

Wiki iliyopita, Hassan alimchagua aliyekuwa waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, kuwa waziri mkuu.

Rais Samia alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa asilmia 98 katika uchaguzi wa Oktoba, lakini zoezi hilo lilikumbwa na maandamano ya kupinga shughuli za uchaguzi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani yanasema mamia ya watu waliuawa katika machafuko hayo, ingawa serikali inapingana na takwimu hizo.

Rais Samia ameahidi kuchunguza vurugu za uchaguzi na siku ya Ijumaa alitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza hadharani kuhusu machafuko hayo, ambayo yamesababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo katika kipindi cha miongo kadhaa.

CHANZO:Reuters
Soma zaidi
Cape Verde, Mauritius na Ushelisheli wafanikiwa kuangamiza surua na  rubela
Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutoka Al Fasher ya Sudan tangu kutwaliwa na RSF
Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri
Tovuti za taasisi za serikali ya Kenya zashambuliwa
Mgodi waporomoka DRC na kuua watu wasiopungua 32
Wahamiaji 4 wafariki baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba makumi ya watu kuzama pwani ya Libya
Kikundi cha matabibu kinaripoti visa ya ubakaji wa wasichana wa Al Fasher baada ya RSF kuteka
Mlipuko wa virusi vya Marburg umethibitishwa kusini mwa Ethiopia
DR Congo, M23 wasaini makubaliano ya amani 'ya kihistoria' nchini Qatar
Baraza la Maaskofu Tanzania lataka uwajibikaji kwa waliohusika na mauaji ya waandamanaji
Baraza la usalama la UN laongezea mwaka mmoja ujumbe wa amani wa Abyei
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC anayeshtakiwa Paris kwa uhalifu wa kivita aanza mgomo wa kula
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi