Kiongozi wa Guinea-Bissau, Jenerali Horta N'Tam, amepandishwa cheo cha meja jenerali — cheo cha juu kabisa katika vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo, kulingana na amri aliyoiweka saini na kutangazwa Alhamisi.
Jeshi lilichukua madaraka Novemba iliyopita, siku chache tu baada ya uchaguzi wa urais wa nchi hiyo, likamuondoa madarakani rais wa zamani Umaro Sissoco Embalo na kusitisha mchakato wa uchaguzi.
Awali, jeshi lilisema litachukua udhibiti kwa muda wa mwaka mmoja na kumteua N'Tam — mshirika wa karibu wa Embalo — kuwa rais wa mpito.
Mpaka sasa, Disemba 6, 2026 ndio imetengwa kuwa siku ya uchaguzi wa urais na wa bunge, unaokusudiwa kurudisha madaraka kwa raia.
Jenerali wa nyota nne
N'Tam awali alikuwa na cheo cha brigedia jenerali. Kwa mujibu wa amri ya Alhamisi, ame "kupandishwa hadi cheo cha meja jenerali," sasa akiwa na nyota nne badala ya mbili.
Jeshi lilidai kuchukua madaraka Novemba ili kuzuia ghasia na umwagikaji wa damu kati ya wafuasi wa wagombea wanaopingana katika uchaguzi. Rais wa zamani Embalo na mgombea wa upinzani Fernando Dias wote walitangaza ushindi wakati ambapo matokeo rasmi yalikuwa hayajatoka.
Kabla ya Novemba, nchi ya pwani ya Afrika Magharibi ilikuwa tayari imepitia mapinduzi ya kijeshi manne na mfululizo wa jaribio la uasi tangu ilipopata uhuru kutoka Ureno mwaka 1974.












