"Badala ya kutoa marufuku kwa TikTok, wizara inapendekeza kupitisha mfano wa ushirikiano wa udhibiti," wizara ya habari na mawasiliano ilisema katika ushauri kwa kamati hiyo, ambayo ilishirikiwa na Reuters siku ya Alhamisi. | Picha: Reuters

Kamati ya bunge imekuwa ikizingatia ombi kutoka kwa raia wa Kenya la kupiga marufuku jukwaa linalomilikiwa na China. Mapendekezo hayo yanafuatia tuhuma kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kwamba jukwaa hilo limetumika kusambaza propaganda, kusambaza uongo, na maudhui yaliyo kinyume na maadili kama vile picha za utupu.

"Badala ya kutoa marufuku kwa TikTok, wizara inapendekeza kupitisha mfano wa ushirikiano wa udhibiti," Wizara ya Habari na Mawasiliano ilisema wakati wa kushauri kamati hiyo, ambayo shirika la Reuters ilishuhudia siku ya Alhamisi.

Wizara ilipendekeza TikTok izingatie yaliyomo ili kuhakikisha yanazingatia sheria za Kenya na kuwasilisha ripoti za robo mwaka kwa serikali kuhusu sehemu walizotoaa kuendana na makubaliano.

TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya China ByteDance, haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni. Kujibu ukosoaji kama huo katika nchi nyingine, kampuni imeshawahi imejitetea kuhusu rekodi yake kuhusu faragha ya mtumiaji.

Kampuni hiyo imekuwa ikikabiliwa na uchunguzi wa udhibiti katika nchi nyingi, hasa nchi za Magharibi.

Mwezi uliopita, Italia iliwapiga faini vitengo vitatu vya TikTok kwa kuruhusu maudhui yanayoweza kuwa hatari kwa watoto au watumiaji.

Seneti ya Marekani ilipitisha sheria siku ya Jumanne ambayo itapiga marufuku TikTok nchini Marekani ikiwa ByteDance itashindwa kuuza ndani ya miezi tisa hadi mwaka ujao.

Reuters