Shirika la ndege la KQ ladai kunyanyaswa na DRC. / Photo: Reuter

Shirika la ndege la Kenya Airways siku ya Ijumaa lilishutumu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa unyanyasaji na kuendelea kuzuia wafanyakazi wawili wa shirika hilo la ndege kwa madai ya ukiukaji wa sheria za forodha licha ya mahakama kuamuru waachiliwe huru.

Afisa mkuu wa serikali ya Kenya pia amekemea kukamatwa kwa wafanyi kazi hao.

Maafisa kutoka idara ya ujasusi ya kijeshi ya DRC waliwazuia hao wafanyakazi wawili Aprili 19 kwa madai ya kushindwa kukamilisha hati za forodha zinazohusiana na mizigo ya thamani ambayo ilitakiwa kusafirishwa wiki moja kabla, shirika hilo la ndege lilisema katika taarifa.

Wafanyakazi hao wa shirika la ndege wamepewa kibali cha ziara moja tu na ziara fupi na ubalozi wa Kenya, shirika la ndege la taifa la Kenya lilisema.

'

Shughuli halali'

Msemaji wa serikali ya Kongo na Wizara ya mambo ya nje hawakujibu kwa haraka walivyo ombwa kutoa maoni.

"Tumesikitishwa na hatua hii inayolenga wafanyakazi wasio na hatia na inachukuliwa kuwa unyanyasaji unaolenga biashara ya Kenya Airways," shirika hilo la ndege lilisema.

Korir Sing'oei, katibu mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje Kenya, alisema serikali imejitolea kulinda raia wake nje ya nchi.

"Kenya inapinga kukamatwa na kuzuiliwa kwa raia wake wanaofanya shughuli za kibiashara kihalali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo," alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Kibali cha forodha

"Misheni yetu huko Kinshasa inajishughulisha kikamilifu na suala hilo."

Wakati wa kukamatwa kwa hao wawili, shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) lilikuwa halijamiliki shehena hiyo kwa sababu mhudumu wa usafirishaji alikuwa bado anatayarisha nyaraka, shirika hilo la ndege lilisema.

"Mzigo huu ulikuwa bado kwenye sehemu ya mizigo ukipitia kibali wakati timu ya usalama ilifika na kudai kuwa KQ ilikuwa ikisafirisha mizigo bila kibali," ilisema.

Mnamo Aprili 25 mahakama ilisema wafanyakazi hao wawili wanapaswa kuachiliwa ili kuruhusu utaratibu unaofaa, shirika la ndege liliongeza.

TRT Afrika