Idhaa ya TRT Español itatoa habari na maudhui yanayolenga hadhira inayozungumza Kihispania, lugha ya msingi inayozungumzwa katika zaidi ya nchi 20 duniani kote.

TRT, shirika la utangazaji la taifa la Uturuki limezindua jukwaa lake la habari la kidijitali la TRT Español kama sehemu ya mkutano wa kwanza wa TRT wa nchi zinazozungumza Kihispania.

"Tunatumaini kuwa TRT Español itakuwa na manufaa kwetu na nchi zote zinazozungumza Kihispania," alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altunm wakati wa shughuli ya uzinduzi wa idhaa hiyo, siku ya Ijumaa jijini Istanbul.

Pia aliongeza kuwa jukwaa hilo ni sehemu ya malengo ya Uturuki kukuza haki kupitia lugha nyingi iwezekanavyo. Altun pia aliapa kuwa vyombo vya habari vya Uturuki vitaendelea "kuwapambania wale wanaoonewa na kuwa sauti ya wanaokandamizwa."

MKurugenzi Mkuu wa TRT Zahid Sobaci pia alihutubia ghafla hiyo na kusema kuwa TRT Español "ni ujio mpya" wa Uturuki kwa Marekani ya Kusini na Hispania.

"Kutoka Hispania mpaka Marekani ya Kusini, Uturuki inaimarisha uhusiano wake wa kikanda," amesisitiza, na kuongeza kuwa TRT inaimarisha uhusiano wake na watangazi wengine wa nchi hizo.

Chini ya kauli mbiu "Mahali Ambapo Watu Ni Muhimu," TRT Spanish inalenga kuunganisha nyanja mbili za kitamaduni na maono huru ya habari, kuwasilisha matukio ya kimataifa kwa mtazamo wa kipekee.

Maudhui mahsusi kwa wazungumzaji wa Kihispania

Mkutano wa Utangazaji wa nchi zinazozungumza Kihispania ulianza Alhamisi kwa warsha kwa wanahabari kutoka nchi zinazozungumza Kihispania.

Warsha hiyo, iliyopewa jina la "Uandishi wa Habari wa Kimataifa," ililenga mada kama vile uandishi wa habari bila upendeleo, matarajio ya umma, uhusiano wa kimataifa, na athari za kisiasa za vyombo vya habari, mijadala ya kuhimiza na kubadilishana mawazo.

Majopo mbalimbali pia yatafanyika Ijumaa alasiri, kuanzia "Kuimarisha Maelewano ya Pamoja kupitia Msururu wa Televisheni: Uturuki na Nchi zinazozungumza Kihispania," hadi "Sura inayobadilika ya Mtiririko wa Habari za Ulimwenguni: Kukuza Sauti ya Nchi zinazozungumza Kihispania kwa Uelewa wa Kimataifa na Usawa."

TRT Español itatoa habari na maudhui yanayolenga hadhira inayozungumza Kihispania, lugha ya msingi inayozungumzwa katika zaidi ya nchi 20 duniani kote.

Hapo awali, TRT ilizindua TRT Francais, TRT Balkan, ambayo inatangaza kwa lugha tatu, na TRT Afrika, ikitangaza katika lugha nne.

TRT Afrika