Hadithi za Kenzera: Zau ni mchezo kitu kipya kwa watu Afrika 

Na Gaure Mdee na Charles Mgbolu

Kuna mchezo mpya unaopatikana Xbox, Playstation 5, Nintendo Switch, na Microsoft Windows PC unaogusia mandhari za kitamaduni za Afrika na kuchezwa kwa Kiswahili.

Hadithi za Kenzera: Zau, ya Muingereza mwenye asili ya Kenya, Abubakar Salim, ni mchezo unaochezwa na kusimuliwa kwa Kiswahili na unafuatilia maisha ya Zau, kijana anayeingia katika dunia mpya inayoitwa Kenzera, ambayo ni dunia tofauti anayofikia akiwa ndotoni na inatokea ili yeye aweze kushawishi roho ambazo kumrudisha baba yake uhai.

Hadithi za Kenzera: Zau

Salim ni muigizaji na mjasiriamali anayeeleza kuwa msukumo wa kutengeneza mchezo huu unatokana na uzoefu wake binafsi wa kupambana na huzuni na maumivu wakati baba yake alipofariki na saratani miaka michache iliyopita.

Changamoto mbali mbali za Zau kwenye mchezo huu ni pamoja na mabonde, maporomoko ya maji, milima na maadui wenye nguvu ambao lazima apigane nao kabla ya kuhamia hatua moja kwenda nyingine.

Wataalamu wa michezo wameumwagia sifa mchezo huu si tu kwamba ni mchezo unaohusisha mapambano na adui, bali pia mandhari nzuri ya Kiafrika ndani ya mchezo huo.

Hadithi za Kenzera: Zau

Michezo ya Kiafrika inavyoweza kuunganisha watu

Black Panther ilikuwa filamu iliyowaunganisha Waafrika kwa njia tofauti na mpya kwa wakati huo na sasa mchezo huu mpya unatoa fursa hiyo.

Wanaocheza huu mchezo wanapata fursa ya kumuona Zau akivuka hatua moja kwenda nyingine iliyojaa mazingira ya kiafrika, kutoka kwa utandaji wa rangi wa nyumba za kifalme zenye utajiri, na mpaka mfano wa jangwa kubwa la Sahara bila kusahau misitu mikubwa ya Afrika.

"Inafurahisha kuona michezo mfano kama hadithi za Kenzara ikisimulia hadithi kutoka mtazamo wa Kiafrika. Ni kama pumzi ya hewa safi. Ni kitu tofauti, kitu cha kipekee zaidi. Hili linawapa watu wa Afrika msukumo wa kujua kwamba wanaonekana kimataifa," Leon Oscar Lwoga, mtengenezaji wa michezo ya kompyuta kutoka Tanzania, anaiambia TRT Afrika.

Hadithi za Kenzera: Zau

"Michezo inasaidia kuwaunganisha watu ambao ni kama wao kwa njia nyingi. Ni vizuri kuona kwamba kuna msisitizo zaidi wa kusimulia mtazamo wa Kiafrika," anaongeza.

Hadithi za Kenzera: Zau

Michezo mingi inayochezwa ni ya soka au ngumi, lakini michezo ya simulizi kama Hadithi ya Zau ni nadra sana kusikia waafrika wakicheza maana hata lugha haiendani na mtiririko mzima wa hadithi na hio inakuwa changamoto kwa mtu asiyeelewa lugha kucheza.

Tales of Kenzera: Zau

"Watu kucheza michezo haujawa maarufu sana barani Afrika; inaweza kuwa njia ya burudani na pia njia ya kusimulia hadithi. Kama filamu na vitabu," anasema Lwoga.

"Inaonesha ulimwengu wote kile tunachoweza kufanya. Nadhani watu wengi kweli hawajui kuhusu bara hili. Pengine wana mtazamo mfinyu au uelewa mdogo wa baadhi ya mambo tunayokabiliana nayo. Wakati ukiwa na michezo iliyotengenezwa na Waafrika kuhusu Waafrika, ni njia kwetu kushiriki historia yetu," anaongeza.

Hadithi za Kenzera: Zau

Sekta ya michezo ya video ulimwenguni ni biashara ya dola bilioni na imekuwa hivyo kwa miaka mingi.

Mwaka 2022, mapato kutoka soko la michezo ya video duniani yalikadiriwa kuwa karibu dola bilioni 347 za Marekani, huku soko la michezo ya simu likizalisha makadirio ya dola bilioni 248 za jumla, kulingana na Statista. Tasnia ya michezo hii imekuwa ikiongoza duniani kwa kuingiza kipato kuliko sanaa zingine.

Katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, idadi ya wachezaji wa michezo hii imeongezeka kutoka milioni 77 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 186 mwaka 2021 kati yao asilimia 40, wakiwa wanapatikana Afrika Kusini.

Hadithi za Kenzera: Zau

"Hii itawahamasisha watengenezaji wengi wa michezo kutoka Afrika kuhisi kama 'ikiwa mtu kama mimi alitengeneza mchezo huu yenye ubora wa juu; nadhani naweza kufanya kitu kama hicho," Lwoga anahitimisha.

TRT Afrika