Makanisa yaliyochongwa Ethiopia / Picha: AFP

Na Coletta Wanjohi

Tunapojenga huwa tunaanzia chini kwenye msingi kwenda juu kwa paa, lakini nchini Ethiopia kuna makanisa 11 ambayo yalichongwa kutoka juu kwenda chini.

Kilomita 645 kutoka jiji la Addis Ababa, katika eneo linaloitwa Lalibela kuna makanisa kumi na moja ya enzi za kati ambayo yalichongwa kwenye miamba.

Inasemekana kuwa Mfalme Lalibela ambaye alianza kujenga katika karne ya 12 alitaka kuunda 'Yerusalemu Mpya', na kuchonga makanisa haya ikatumia muda wa miaka 23 kukamilika.

Lalibela ni maarufu kwa makanisa yake yaliyochongwa kwenye miamba. / Picha: Reuters.

Inakadiriwa ilichukua miaka 24 kujenga makanisa yote 11 yaliyochongwa kwenye miamba.

Makanisa hayakujengwa kwa njia ya kitamaduni bali yalichongwa kutoka kwa mwamba, kwa kiingereza inaitwa monolithic. Vitalu hivi vilitobolewa zaidi, na kutengeneza milango, madirisha, nguzo, sakafu mbalimbali, paa na kadhalika.

Yalichongwa ndani na nje kutoka kwenye mwamba mmoja.

Kati ya hiyo 11, 4 yanajisimamia kwa mwamba mmoja mmoja na 7 yameshikiliwa kwa ukuta na mlima yalipochongewa.

la Lalibela bado inatumiwa na Kanisa la Kikristo la Kiorthodoksi la Ethiopia hadi leo. / Picha: A A

Kwa wakristu wafuasi wa dini ya Othodoksi hili ni eneo muhimu kwao na maelfu huja hapa kila mwaka kwa maombi.

Eneo hili la Lalibela bado inatumiwa na Kanisa la Kikristo la Kiorthodoksi la Ethiopia hadi leo, na inasalia kuwa mahali muhimu pa kuhiji kwa waumini wa Othodoksi wa Ethiopia.

Shirika la UNESCO limetambua makanisa ya Lalibela kama urithi wa dunia tangu 1978.

UNESCO limetambua makanisa ya Lalibela kama urithi wa dunia tangu 1978. / Picha: Reuters

Ubunifu huu wa kuvutia umegeuza mji huu wa mlima wa lalibela kuwa mahali pa fahari ikiwa kivutio cha wageni 80,000 hadi 100,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa waumini wa Kanisa la Othodoksi la Ethiopia ambao huja hapa kila mwaka kuhiji.

Watu wengine wanakuja kushangaa jinsi ambavyo majengo haya makubwa yalivyochongwa tu na kuwa majengo ya namna hii?

TRT Afrika