Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa mchakato wa usambazaji wa chakula kwa Wapalestina umezorota kutokana na ukaguzi mwingi unaofanywa na Israel./ Picha: AFP  

Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ameonya uwezekano wa kuwepo uhaba mkubwa wa chakula kaskazini mwa Gaza na kutoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi ya Israeli dhidi ya Wapalestina.

"Kuna baa la njaa, baa kubwa la njaa, katika eneo la Kaskazini huku likielekea upande wa kusini," amesema Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo kupitia mahojiano.

"Tunachokiomba, na ndicho tunachoendelea kuomba ni usitishwaji wa mashambulizi na uwezekano wa kupitisha misaada kirahisi katika eneo la Gaza," ameongeza McCain.

Shirika hilo ni kati ya taasisi nyingi duniani zinazojaribu kufikisha misaada katika eneo la Gaza.

Siku ya Ijumaa, Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula katika eneo la Gaza imeimarika kidogo, licha ya baa la njaa kuendelea kulikumba eneo hilo dogo lenye watu milioni 2.4.

TRT Afrika