#KUH85 : Fighting in Khartoum amid rivalry between generals / Photo: AFP

Mataifa ya Kiafrika yanaharakisha kuwahamisha raia wao kutoka Sudan ambako mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi na kundi la wanamgambo wanao udhibiti mji mkuu, Khartoum.

Wanajiunga na orodha inayo ongezeka ya nchi ambazo zimekuwa zikifanya shughuli za uokoaji kwa njia ya bahari na anga kwa wanadiplomasia wao na raia tangu Jumamosi.

Mashambulizi ya mabomu na milio ya risasi ya wiki moja katika jiji hilo yamesababisha vifo vya mamia na maelfu kujeruhiwa.

Nigeria na Ghana zilisema zinafanya kazi ya kuwaondoa raia wao kupitia nchi jirani.

Nigeria ilisema inapanga kuwahamisha raia 5,500 - wengi wao wakiwa wanafunzi - kwa barabara kuelekea Misri kwa sababu ya hatari inayoweza kutokea katika anga ya Sudan.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni Geoffrey Onyeama alisema uondoaji huo utaanza mara tu serikali ya Sudan itakapo hakikisha usalama na njia salama itawekwa.

Alisema baadhi ya wanadiplomasia watasalia Khartoum kuandaa uhamisho huo huku ubalozi wa nchi hiyo ukiwashauri wanafunzi hao kukaa majumbani.

"Ni wazi, unachohitaji katika hali kama hii ni mahali ambapo kila mtu anaweza kukusanyika kabla ya kuanza kuwahamisha.

Wizara ya mambo ya nje ya Ghana ilisema idadi ya raia wake, haswa wanafunzi, waliathiriwa na mzozo huo lakini wote walisemekana kuwa salama. Ilisema ubalozi wake nchini Misri unashughulikia kupata njia salama ya kuelekea Ethiopia.

Katika taarifa ya ubalozi huo, uliwaambia familia na marafiki wa raia wa Ghana waliokwama nchini Sudan kwamba "kila juhudi zinafanywa kuhakikisha usalama wa wapendwa wao hadi watakapo wasili Ghana".

Kutatizika kabisa kwa huduma ya intaneti kulithibitishwa Jumatatu na Netblocks, kikundi cha ufuatiliaji wa mtandao, ambacho kilitaja madai ya kijeshi kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi vinadaiwa kuhujumu ubadilishanaji wa mawasiliano ya simu.

Raia wengi wa Kiafrika waliokwama na vikundi vya wanafunzi wamekuwa wakitegemea mtandao kufikia wanadiplomasia na familia zao nyumbani.

Vurugu zinazoendelea zimeathiri shughuli katika uwanja mkuu wa kimataifa wa ndege, kuharibu ndege za raia na kuharibu angalau njia moja ya ndege, na moshi mzito na mweusi ukapanda juu yake.

Viwanja vingine vya ndege pia vimezuiwa kufanya kazi.

TRT Afrika