Maliha alijozeelea umaarufu kufuatia jaribio lake la pili./Picha: 

Na

Charles Mgbolu

Mitandao ya kijamii imetekwa na Wakenya wengi wakimshangilia mpishi maarufu wa Kenya Maliha Mohammed aliyepika kwa saa 150 mwezi Novemba.

Kilichobaki ni uthibitisho kutoka kwa waandalizi wa tuzo za Guinness kujua kama Maliha aliweka rekodi mpya.

Lakini haikuwa hivyo, kwani Maliha alichapisha habari za kuhuzunisha kwenye Instagram kwamba alikuwa amekataliwa na bodi ya rekodi.

''Ni kwa masikitiko makubwa kwamba ninawajulisha familia yangu, marafiki, mashabiki, wafadhili, wafuasi, na kila mtu ambaye alionyesha upendo na kuniunga mkono kuelekea safari yangu katika mbio za marathoni za kupika za Novemba... ,'' aliandika kwenye Instagram siku ya Jumamosi.

Sheria kali za kuvunja rekodi

Katika taarifa yao, Guiness wanasema kuwa Maliha alipumzika zaidi tofauti na utaratibu.

"Kwa bahati mbaya, hairuhusiwi kutengeneza mapumziko kwani ni lazima limbikizwe tu. Kwa maslahi ya haki kwa waombaji wote, tunaweza tu kuidhinisha rekodi wakati miongozo yote imefuatwa kikamilifu,'' ilisema katika taarifa.

''Tunashukuru kwamba hii ni habari ya kukatisha tamaa kupokea lakini tunatumai haitakuzuia kutoka kwa rekodi za siku zijazo,'' taarifa yao iliongeza.

Jitihada za kurudia

''Siko sawa kwa sasa. Naomba msamaha wako kwa kuwaangusha nyote,’’ alisema Maliha.

Maliha amesifiwa kwa kwa ujasiri wake. Picha: Maliha/Instagram

Maliha alitumia saa 90 na dakika 15 katika jaribio lake la kwanza la 2023, lakini hakuwahi kupata nafasi ya kudai ushindi huo kwani mpishi wa Nigeria Hilda Baci aliruka mnamo Novemba kupika kwa saa 93 na dakika 11 na kudai rekodi hiyo.

Maliha alikuwa na matumaini kwamba jaribio lake la pili katika rekodi ambayo sasa inashikiliwa na mpishi wa Ireland Alan Fisher lilikuwa na uhakika kwamba uthibitisho wa rekodi yake ulikuwa wa uhakika, lakini hatima ilikuwa na mawazo tofauti.

‘’Haikuwa rahisi ila najua Mungu ana mipango mingine na mimi in shaa Allah maana kilichokusudiwa utakipata kirahisi. Kwa wale waliokuwa wakisubiri rekodi hii, samahani sana,’’ aliandika kwenye mitandao ya kijamii.

Mwitikio kutoka kwa mashabiki umekuwa mwingi wa uungwaji mkono.

Mpishi Maliha/Instagram.

“Wewe bado ni shujaa kwetu; hii ni ishara tu ya kuiendea kwa njia bora, usikate tamaa; kuna milango mingine itafunguka, na tunaendelea nayo,’’ aliandika shabiki mwingine, Jevaney, pia kwenye Instagram.

Rekodi za Dunia za Guiness zina idadi kubwa ya sheria kali ambazo lazima zifuatwe kwa mafanikio yetu yote yaliyovunja rekodi.

‘’Tunatathmini majina yote mapya ya rekodi dhidi ya maadili yetu ya uadilifu, heshima, ushirikishwaji, na shauku, na ni muhimu sana kwetu kwamba rekodi zetu zote zinaonyesha hili,’’ Guiness World Record inasema.

Miezi miwili iliyopita, matumaini ya mwanahabari wa Ghana Afua Asantewaa kuingia katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness kwa mbio ndefu zaidi za kuimba na mtu binafsi yalikwama baada ya kutangazwa kuwa ameondolewa.

Afua Asantewaa alivumilia mbio za marathon za siku tano ambazo zilianza usiku wa manane Jumapili, Desemba 24, na kuhitimishwa saa 7:00 asubuhi mnamo Desemba 29. Aliimba kwa saa 126 na dakika 15.

Maliha hajaonyesha kama atakuwa anafanya jaribio la tatu la kuvunja mbio ndefu zaidi za upishi na mtu binafsi, na kumwacha mpishi wa Ireland Alan Fisher bado akinyakua taji.

TRT Afrika