The Nairobi skyline is seen in the background as rhinos graze in the Nairobi National Park, near Nairobi / Photo: Reuters

Kenya, nchi ya Afrika Mashariki, imeorodheshwa kama nchi bora zaidi barani Afrika kwa wahamiaji na Shirika la The InterNations' Expat Essentials Index, ambalo linaorodhesha nafasi ya juu hadi ya chini zaidi duniani kote.

Vigezo vilivyotumika ni, viwango vya urahisi wa kuanza maisha, maisha ya kidijitali, urahisi wa kupata nyumba na gharama za nyumba yenyewe, hadi lugha zinazo zungumzwa. Kiingereza na Kiswahili ndizo lugha zinazozungumzwa na watu wengi zaidi Kenya, ambayo ina wakazi wapatao milioni 50.

Kenya sasa imeorodheshwa ya tisa duniani, ikizipita Afrika Kusini (iliyorodheshwa ya 28) na Misri ( iliyoorodheshwa ya 37), ambazo zote zimeshikilia nafasi ya kwanza kwa miaka kadhaa iliyopita.

Viwango hivi viliiweka Kenya kuwa eneo la kuvutia kwa mhamiaji, mwekezaji, au kampuni yoyote ambayo ingependa kuweka msingi katika nchi hiyo.

Kwa mtaalam yeyote kutoka nje ya nchi, ubora na mambo muhimu ya maisha, pamoja na urahisi wa kusuluhisha jinsi ya kushughulikia fedha za kibinafsi, ni miongoni mwa mambo yanayotatiza, hasa katika nchi yoyote ya Kiafrika.

Maeneo ya kifahari ya Westlands, Runda, Muthaiga, Kilimani, Lavington, na Karen yanavutia idadi kubwa ya wahamiaji kutoka nje.

Nchi hiyo pia ilitajwa kuwa nchi ya juu ya uwekezaji wa mali isiyohamishika na kampuni uwekezaji ya Knight Frank, mbele ya Italia, Uingereza, na Ufaransa.

Bahrain inashika nafasi ya kwanza duniani kwa mwanzo rahisi. Ujerumani imeorodheshwa chini kati ya nchi 52 kwa sababu wahamiaji wanakabiliwa na vikwazo vingi vinavyo katisha tamaa nchini humo.

TRT Afrika