| Swahili
MICHEZO
5 DK KUSOMA
Timu 20 bora za Kiafrika kulingana na viwango vya hivi karibuni vya FIFA
Morocco ndiyo timu ya soka ya wanaume iliyoorodheshwa bora zaidi barani Afrika, kulingana na viwango vya hivi karibuni vya FIFA
Timu 20 bora za Kiafrika kulingana na viwango vya hivi karibuni vya FIFA
Senegal inashika nafasi ya pili, Misri inashika nafasi ya tano na Cameroon nafasi ya saba katika soka la Afrika, kwa mujibu wa FIFA. / Picha: TRT Afrika / Others

Morocco inaendelea kuongoza Afrika kama timu ya soka ya wanaume iliyoorodheshwa zaidi barani humo, kulingana na viwango vya hivi punde vya FIFA vilivyotolewa Alhamisi.

Washindi wa nusu fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 wameorodheshwa katika nafasi ya 13 ulimwenguni, nyuma ya Argentina, Ufaransa, Brazil, England, Ubelgiji, Ureno, Uholanzi, Uhispania, Italia, Kroatia, USA na Mexico kwa mpangilio huo.

Morocco ilikuwa na pointi 1658.49, pointi 5.45 nyuma ya Mexico iliyo nafasi ya 12.

FIFA hutumia fomula changamano ya kukokotoa pointi ambayo ilifanyiwa marekebisho Septemba 2023.

Kwa maneno rahisi, shirikisho la soka duniani hupanga timu kulingana na jumla ya pointi zilizopatikana katika mechi za mashindano katika kipindi fulani.

Tano bora

Kwa hivyo, timu iliyo na viwango bora imekuwa na matokeo mazuri katika siku za hivi karibuni ikilinganishwa na ile iliyo na nafasi ya chini.

Mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 Senegal wanashika nafasi ya pili barani Afrika, na nafasi ya 20 duniani kote, wakiwa na pointi 1600.82.

Tunisia, ambayo inashika nafasi ya 32 duniani, iko nafasi ya tatu barani Afrika ikiwa na pointi 1516.14.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini linafuatwa na majirani zake Algeria, ambao wapo katika nambari 33 duniani, wakiwa na pointi 1512.9.

Misri inamaliza timu tano bora za soka barani Afrika, ikiwa na pointi 1511.95, na kuwaweka katika nafasi ya 35 duniani.

Burkina Faso yatinga 10 bora

Nigeria ni ya sita barani humo na ya 40 duniani ikiwa na pointi 1490.48.

Cameroon iko nafasi ya saba barani Afrika na ya 43 duniani ikiwa na pointi 1466.98, ikifuatiwa na Mali iliyo katika nafasi ya 47 duniani kwa pointi 1449.75.

Wenyeji wa AFCON 2023 Côte d'Ivoire - au Ivory Coast - wako katika nafasi ya tisa barani Afrika, na ya 52 ulimwenguni kwa alama 1439.17.

Burkina Faso, ambao wameorodheshwa katika nafasi ya 56 duniani kote, wanakamilisha timu kumi bora za soka barani Afrika kwa pointi 1410.59.

Eritrea haijaorodheshwa

Timu zote za Afrika ziliorodheshwa na FIFA, isipokuwa Eritrea, ambayo shirikisho la soka duniani linasema, ilishindwa kucheza mechi za kawaida.

"Hakuna nafasi (kwa Eritrea) kutokana na kutocheza angalau mechi moja katika kipindi cha miezi 48 iliyopita au kutocheza angalau mechi tano dhidi ya timu zilizoorodheshwa rasmi," FIFA ilisema Alhamisi.

Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya timu za Kiafrika na FIFA kufikia Oktoba 2023:

1. Morocco (13 duniani kote)

2. Senegal (20)

3. Tunisia (32)

4. Algeria (33)

5. Misri (35)

6. Nigeria (40)

7. Cameroon (43)

8. Mali (47)

9. Côte d'Ivoire (52)

10. Burkina Faso (56)

11. Ghana (60)

12. Afrika Kusini (64)

13. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (65)

14. Cape Verde (74)

15. Guinea (80)

16. Zambia (81)

17. Gabon (86)

18. Uganda (90)

19. Guinea ya Ikweta (91)

20. Benin (93)

21. Mauritania (101)

22. Jamhuri ya Kongo (106)

23. Madagascar (108)

24. Kenya (110)

25. Guinea-Bissau (110)

26. Msumbiji (113)

27. Namibia (114)

28. Angola (116)

29. Gambia (117)

30. Togo (119)

31. Tanzania (121)

32. Sierra Leone (122)

33. Malawi (123)

34. Zimbabwe (125)

35. Libya (126)

36. Jamhuri ya Afrika ya Kati (127)

37. Komoro (128)

38. Niger (129)

39. Sudan (130)

40. Rwanda (140)

41. Burundi (142)

42. Ethiopia (143)

43. Eswatini (zamani Swaziland) - 146

44. Botswana (148)

45. Liberia (151)

46. Lesotho (153)

47. Sudan Kusini (167)

48. Mauritius (177)

49. Chad (179)

50. Sao Tome na Principe (186)

51. Djibouti (189)

52. Ushelisheli (195)

53. Somalia (196)

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Lamine Yamal: Mfalme aliyekosa taji la Ballon d'Or
Ukraine yapinga uamuzi wa kuipa Moscow uwenyeji wa Mashindano ya kunyanyua vyuma 2030
Kenya yafuzu hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la U-17 kwa mara ya kwanza
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa CAF, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wabanduliwa
Kombe la Dunia la Wanawake la U-17: Nigeria yaitungua mabingwa watetezi Korea Kaskazini
Marekani mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Wanawake Kombe la Dunia la Klabu FIFA 2028
Liverpool yapindua meza dhidi ya Villarreal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
CAF yazindua kombe jipya kuelekea Ligi ya Mabingwa ya Wanawake nchini Misri
Zambia na Ghana zapata vipigo katika Kombe la Dunia la Wanawake la U-17
Goli la dakika za mwisho la Madueke lawapa Arsenal ushindi dhidi ya Nottingham Forest
Morocco yaanza kwa ushindi huku Nigeria ikifungwa na Poland katika Kombe la Dunia la Wanawake  U-17
Kombe la Dunia toleo la 10 kwa wanawake U-17 kuanza nchini Morocco
Fifa yaitoza faini Hispania kwa semi za chuki dhidi ya Uislamu wakati wa mechi ya kirafiki na Misri
Infantino aomba radhi kuhusu mpango wa kubinafsisha haki za kibiashara za FIFA
Winga wa zamani wa Barcelona, Chelsea Pedro astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39
Ronaldo Ruhsa kurejea kwenye timu kama itampendeza: kocha
Manchester City watapewa adhabu gani?
Rais wa FIFA Infantino aahidi fedha zaidi kwa mashirikisho
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani