Mchezaji nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo anaweza kurejea kwenye timu hiyo kama akitaka, licha ya kuondoka, amesema kocha wa timu ya taifa Jorge Jesus siku ya Jumapili.
Jesus alisema Ronaldo anaweza kurejea "kama anataka" baada ya timu kuifunga Norway bila ya mshambuliaji huyo na kufanikiwa kufika robo fainali ya Ligi ya Mataifa UEFA.
Mtafaruku huu ulianza wiki iliopita wakati Jesus alipomuacha nje ya kikosi Ronaldo mwenye umri 41 ikiwa ni ushindi wa kwanza wa Ureno dhidi ya Norway. Ronaldo aliondoka kwenye timu hiyo siku ya Jumatano baada ya kubaini kuwa hatocheza kweye mechi dhidi ya Denmark.
"Kwangu mimi, Cris, yuko kwenye mipango yangu, kama anacheza Al-Nassr, atakuwa mchezaji ambaye naweza kumjumuisha," Jesus aliwaambia waandishi wa habari, akizungumzia klabu ya Ronaldo ya Saudi Arabia. "Akitaka, anaweza kurejea kwenye timu ya taifa."
‘Ronaldo afanye maamuzi’
Kocha anasema kama Ronaldo anataka kuzungumza na yeye kabla ya mechi inayofuata ya Ureno mwezo Novemba, hilo litafanyika.
"Akitaka, kama tulivyozungumza kabla ya kumuita, tulizungumza kabla ya kumuita, tunaweza kuzungumza sasa kabla sijamuita kwa mechi inayofuata," aliendelea Jesus. "Lakini Cris ndiyo ataamua kuhusu hilo."
Ronaldo, ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Manchester United ndiye mfungaji bora zaidi wa timu ya taifa ya Ureno na pia aliyecheza mechi nyingi kwa timu hiyo.
Jesus alisema kuwa alimwambia Ronaldo kuwa anamhitaji kwenye timu hiyo katika mechi za kwanza baada ya kumrithi kocha Roberto Martinez kufuatia michuano ya Kombe la Dunia 2026.



















