Momodou Taal, ni mwanafunzi wa Shahada ya Udaktari mwenye asili ya Gambia na Uingereza.
Akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Cornell, Taal anachukizwa na udhalimu unaoendelea Gaza.
"Palestina imeshika kioo na kuiuliza dunia, tunatakiwa tuishi kwenye ulimwengu upi?" anasema katika mahojiano yake na TRT Afrika.
Wakati Taal na watu wengine wengi, wanasaka majibu na kuendelea kuonesha mshikamano na watu wa Palestina, wengine, hasa wa nchini Marekani wanakabiliana na mambo wasiotarajia.
Utawala wa Rais Donald Trump ulibatilisha vibali vya wanafunzi 300, hususani wale walioshiriki maandamano ya kuiunga mkono Palestina.
Kati ya hao, ni Rumeysa Ozturk raia wa Uturuki.
Kwa upande wake, Taal alitakiwa ajisalimishe kwenye mamlaka za uhamiaji baada ya kulalamikia kubatilishwa kwa kibali chake.
"Tunaelewa maana ya vita dhidi ya ubepari na ukoloni na namna Marekani inavyotekeleza mambo yake," anasema Taal ambaye amekwisha ondoka nchini Marekani.
Mwangwi wa kikoloni
Hata hivyo, mwangwi wa maoni ya Taal ulivuma wakati wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah wa Namibia aliweka bayana kuwa nchi yake ilipitia udhalimu wa mauaji ya kimbari ya kwanza kabisa katika karne ya 20.
Pia, alionya kuwa itakuwa ni mwendelezo wa uonevu wa kihistoria kushindwa kutatua mzozo wa Palestina.
Taal anasisitiza kuwa lugha ya Israel inayotumika dhidi ya Wapalestina inaakisi sauti moja ulimwenguni.
"Ingekuwa umuondoe mtu anayezungumza basi ungedhani uko kwenye karne ya 16."
Ukaribu na Palestina
Palestina tunayoiona siku hizi ilikuwa ni mali ya utawala wa Ottoman zaidi ya karne moja iliyopita.
Baada ya kuanguka kwa utawala huo wakati wa vita ya kwanza ya dunia, uingereza ilishika hatamu.
Mwaka 1917, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Arthur James Balfour, aliwaunga mkono Wayahudi ndani ya Palestina.
Taal anamnukuu Profesa wa Siasa za Kiarabu kutoka Chuo Kikuu cha Columbia Joseph Massad, akionesha namna Palestina ilivyokuwa na bahati mbaya ya kuwa koloni la kwanza na la mwisho la Uingereza.
Mauaji ya wayahudi yalisababisha watu hao kuhamia Palestina, wakikimbia utawala wa Nazi.
Baada ya vita kuu ya pilu ta dunia, Baraza Kuu La Umoja wa Mataifa lilipiga kura ya kuigawa Palestina kati ya Waarabu na Wayahudi, mnamo Novemba 29, 1947.
Kuanzishwa kwa Israel, kulisababisha vita na majirani zake katika nchi za Kiarabu.
Palestina iliita vita hivyo "al Naqba", yaani janga.
Watu wapatao 700,000 walipoteza makazi yao.
Mjadala wa Oktoba 7
"Tukumbushwe kuwa historia haianzii Oktoba 7,” anasema Taal.
Hata hivyo, si kila mtu mwenye kukubaliana na dhana hii. Msemaji wa jumuiya ya Waebrania Weusi waishio Israel anasisitiza “kulikuwa na hali ya uhasama hapo kabla. "
"Makombora yaliyotumwa Dimona yamesababisha uharibifu mkubwa," anasema Moore.
Wakati viongozi wakitafuta suluhu ya kisiasa Moore anapendekeza mawazo tofauti kidogo.
"Tunachopaswa kutafuta ni suluhu la kiroho lenye msingi wa kanuni za kimsingi na sifa za Mungu - upendo, huruma, ukweli na amani," anaiambia TRT Afrika.