| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki kuanza uchimbaji wa petroli Pakistan, Waziri wa Mambo ya Nje Fidan anasema
Uturuki na Pakistan wanatarajiwa kuimarisha uhusiano wao wa kimkakati kwa kutia saini makubaliano ya nishati ya uchimbaji mafuta na gesi, pamoja na kupanua biashara, ushirikiano wa masuala ya ulinzi, na maeneo maalum ya kiuchumi kwa wawekezaji.
Uturuki kuanza uchimbaji wa petroli Pakistan, Waziri wa Mambo ya Nje Fidan anasema
Makampuni ya Uturuki ya Pakistan yataweza kwa pamoja kuendeleza uchimbaji wa mafuta na gesi nchini Pakistan. (Picha: AA) / AA
9 Julai 2025

Makampuni ya Uturuki yatachimba mafuta na gesi katika visima vya Pakistan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alisema wakati wa ziara rasmi mjini Islamabad.

Akizunguma wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Pakistan na Waziri wa Mambo ya Nje Muhammad Ishaq Dar siku ya Jumatano, Fidan alisisitiza kuwa nia ya Uturuki ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nishati na Pakistan, hasa katika sekta za kimkakati.

"Uturuki na Pakistan wanafanya kazi pamoja kwa lengo la kuimarisha kiwango cha biashara hadi dola bilioni 5," Fidan alisema. "Pia tunatathmini ushirikiano katika maeneo muhimu ikiwemo madini, mafuta, gesi asilia, na vile vinavopatikana ardhini."

Fidan alieleza kuwa makubaliano ya nishati yaliyotiwa saini mwezi Aprili kati ya Shirika la Petroli la Uturuki (TPAO) na Kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Pakistan kuwa “ni hatua muhimu ya maendeleo” kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

Kutokana na makubaliano haya, Makampuni ya Uturuki na Pakistan yatashirikiana katika uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo ya Pakistan—jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya ushirikiano wa nishati kati ya Uturuki na Pakistan.

“Hii ni moja ya matokeo ya mtazamo huo wa kitaasisi ambao tunalenga kuanzisha,” aliongeza.

Kuimarisha ushirikiano  

Ishaq Dar alisema Pakistan na Uturuki wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbali mbali, ikiwemo uchumi, sekta ya ulinzi, nishati, na miundombinu.

Akipongeza sekta ya ulinzi ya Uturuki, Dar alisema Pakistan inalenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na katika sekta ya ulinzi pamoja na kuendeleza amani na uthabiti katika kanda.

Pande zote hizo mbili "kwa dhati kabisa" zinashirikiana katika masuala mbali mbali, ikiweo kubadilishana mawazo ya kukabiliana na ugaidi, alisema Dar.

Makampuni ya Uturuki pia yatashiriki katika ubinafsishwaji wa sekta ya umeme, aliongeza.

Maeneo maalumu ya kiuchumi

Pande zote mbili, Dar alisema, zinafuatilia kuanzishwa kwa maeneo maalum ya kiuchumi kwa ajili ya wajasiriamali katika miji ya Karachi na Istanbul.

"Tunafuatilia kuhusu kufaidika kutoka kwa uzoefu wa Uturuki na utaalamu wao katika masuala ya biashara ya meli, na matumizi sahihi ya maji kwa ajili ya kilimo," Dar alisema.

Alisema Pakistan na Uturuki wamekubaliana kuhusu tume ya mawaziri ya pamoja baada ya miaka 11, ambayo itakuwa na wenyeviti wenza Waziri wa Biashara wa Pakistan Jam Kamal na Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler.

"Juhudi zote hizi zitaweka msingi wa kongamano la nane la Baraza la Ushirikiano wa Kimkakati," ambalo litafanyika mwaka ujao nchini Uturuki, aliongeza.

CHANZO:TRT World and Agencies
Soma zaidi
Rais Erdogan wa Uturuki alaani shambulizi dhidi ya Azerbaijan
Erdogan: Uturuki itatumia jitahada zote kulinda mipaka na anga zake
NATO yatungua kombora la Iran lililokuwa limeelekezwa Uturuki
Turkish Airlines yaongeza idadi ya ndege
Mashambulizi dhidi ya Iran ni ya haramu
Uturuki inatoa wito kwa Marekani, Israel, Iran kusitisha mapigano mara moja
Fidan amejadili na wenzake wa Pakistan na Afghanistan kuhusu mzozo kati ya nchi hizo mbili
Shirika la Uturuki lapeleka msaada wa chakula kwa familia 8,250 zinazokumbwa na ukame Somalia
Rais Erdogan atuma rambirambi kwa watu wa Azerbaijan wanaoadhimisha miaka 34 tangu mauaji ya Khojaly
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na wanadiplomasia wa OIC mjini Ankara, asisitiza umoja
Israel yaishambulia Gaza na Ukingo wa Magharibi licha ya makubaliano ya kusitisha vita: Erdogan
Erdogan atangaza kuanza kwa uchunguzi kufuatia ajali ya ndege ya kivita ya F-16 ya Uturuki
Erdogan: Uhuru wa kidijitali ni sehemu muhimu ya usalama  wa taifa
Erdogan apongeza kuimarika kwa sifa ya Uturuki duniani asisitiza mpango wa ‘Uturuki isiyo na ugaidi'
Pakistan, Uturuki zaahidi ushikiriano zaidi wa ulinzi huku maafisa waandamizi wakiitembelea Ankara
Rais Erdogan atuma salamu za Ramadhan kwa taifa na ulimwengu wa Kiislamu
Mifumo ya usalama ya Ulaya 'haitofanikiwa' bila Uturuki: Erdogan
Uturuki inaadhimisha miaka 74 katika NATO na tasnia inayokua ya ulinzi
Uturuki kuwa na miradi 'madhubuti' na Ethiopia katika umeme na nishati
Erdogan: Kwa Israel kutambua Somaliland hakutamfaidi yeyote