| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mkenya anayeshukiwa kufanya biashara haramu ya siafu akamatwa
Inadaiwa mshtakiwa huyo alisambaza siafu hao mnamo Aprili 2025 kwa washukiwa watatu wa Vietnam, Mbelgiji, na Mkenya, ambao walikamatwa na kushtakiwa katika mahakama ya JKIA
Mkenya anayeshukiwa kufanya biashara haramu ya siafu akamatwa
Mkenya Charles Mwangi anashukiwa kusamabza siafu kwa njia isiyo halali / Picha:@ODPP_KE / Public domain
tokea saa limoja

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) nchini Kenya alimshtaki mwanamume anayeshukiwa kusambaza siafu hai kwa wageni kwa njia haramu.

Nchini Kenya ni kinyume cha sheria kusafirisha siafu kutoka Kenya bila idhini sahihi.
Siafu wana soko kubwa huko Asia na Ulaya ambapo mazoeea ya kuweka siafu yanakua kwa kasi.

Mshukiwa Charles Mwangi alifikishwa katika mahakama jijini Nairobi baada ya polisi kufanya upekuzi katika nyumba yake na kupata vifurushi vidogo vdofo 1000 vilivyokuwa na siafu hai wa bustani, na wengine 113 wakiwa wamefungwa kwenye chupa ya glasi na siafu 503 wakiwa katika sindano.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa baada ya kukamatwa kwa mshukiwa, ufuatiliaji zaidi ulifanyika katika hoteli moja ndani ya mji wa Nakuru, ambapo ilithibitishwa kupitia camera za CCTV kuwa mshukiwa alisambaza siafu hao kwa raia wa China
kwa jina Zhang Kequn 5 Machi 2026.

Upande wa mashtaka ulimhusisha mshukiwa huyo kwa kusambaza shehena ya siafu ambayo ilikamatwa Bangkok tarehe10 Machi 2026, ambayo ilitoka Mombasa,

Mwangi anadaiwa kuwa na uhusiano mkubwa na washirika walioko kaunti za Naivasha
Mombasa na Kajiado nchini Kenya.

"Mshtakiwa alisambaza siafu hao mnamo Aprili 2025 kwa washukiwa watatu wa Vietnam, Mbelgiji, na Mkenya, ambao walikamatwa na kushtakiwa katika mahakama ya JKIA," mwendesha mashtaka aliiambia mahakama.

Hakimu Mkuu Mwandamizi Irene Gichobi aliagiza mshukiwa azuiliwe kwa siku tatu kuruhusu uchunguzi kukamilika. Kesi hiyo itatajwa tena Machi 19, 2026.

CHANZO:TRT Swahili