Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Among, ameitaka Serikali kueleza sababu za ugawaji wa matrekta yasiyo na majembe kwa wakulima wa Kaskazini mwa nchi.
Ameiuliza serikali iwapo matrekta hayo ambayo sasa hayatumiki yalitolewa kwa madhumini gani.
"Serikali, mlitoa matrekta bila kutoa majembe, hiyo ilikuwa kwa ajili ya mapambo?" aliuliza Spika Katika kikao cha Bunge siku ya Jumatano.
Hii ilifuatia malalamiko yaliyotolewa na Christopher Komaketch mbunge wa kaunti ya Arua ambaye aliilaumu serikali kwa kushindwa kutoa majembe kwa matrekta yaliyopewa wakulima Kaskazini mwa Uganda.
“Spika, ulitoa tangazo kuhusu matrekta ambayo yalisambazwa Kaskazini mwa Uganda na Rais. Na tamko lilikuwa wazi, kwamba Waziri wa Kilimo na Waziri wa Fedha wahakikishe kwamba matrekta ambayo walipewa wakulima wa Kaskazini mwa Uganda, hasa kanda ndogo ya Acholi na wilaya ya Pader wamepata majembe,” Komaketch amesema.
“Hadi leo, matrekta yameegeshwa, yana kutu, na wakulima wadogo wanaangalia tu matrekta ambayo hayatumiki. Naomba uelekeze matrekta yapatiwe majembe ili wakulima waendelee na shughuli zao,” ameongezea.
Mbunge huyo amesema hii imesababisha matrekta hayo kukaa bila kutumika katika makao makuu ya wilaya, ilhali bado wakulima wadogo wanayahitaji kwa ajili ya mashamba yao.
Mario Obiga, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo ya Miji alijitolea kuifahamisha Wizara ya Kilimo juu ya wasiwasi uliotolewa na wabunge ili kutoa msimamo wa hivi punde kwa nini majembe bado hayajatolewa.
"Sio katika mkoa wa Acholi pekee, lakini katika maeneo mengi ya nchi, matrekta haya yalitolewa na Waziri aliahidi kwamba wangenunua majembe na hili halijafanyika. Ninajitolea kumfahamisha Waziri kuhusu uharaka wa jambo hili ili aje Bungeni na kutupa msimamo wa hivi punde,” Waziri Obiga aliliambia Bunge.


.jpg?width=720&format=webp&quality=80)



.jpg?width=128&format=webp&quality=80)








.jpg?width=512&format=webp&quality=80)













