| swahili
Benki Kuu ya Tanzania yatangaza bei ya ununuzi wa dhahabu
Chini ya mpango huo, BOT inasema kuwa wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuiuzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu.
Benki Kuu ya Tanzania yatangaza bei ya ununuzi wa dhahabu
Kulingana na taarifa hiyo iliyotolea Oktoba 18, 2024, kutakuwa na malipo ya asilimia 100 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji wa madini hayo./Picha:  @yose_hoza
18 Oktoba 2024

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetangaza bei ya ununuzi wa madini ya dhahabu.

Kwa mujibu wa tangazo lilitolewa na benki hiyo itanunua madini hayo kwa gharama ya dola za kimarekani 87 (Shilingi za Kitanzania 237, 101.26) kwa gramu moja ya dhahabu.

Kulingana na taarifa hiyo iliyotolea Oktoba 18, 2024, kutakuwa na malipo ya asilimia 100 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji wa madini hayo.

“Muda wa malipo ni saa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji,” tangazo hilo lilisema.

Chini ya mpango huo, BOT inasema kuwa wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuiuzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu.

“Wauzaji wa dhahabu wanapaswa kuwasilisha dhahabu yao katika viwanda vilivyoainishwa ambavyo ni Geita Gold Refinery Limited, Mwanza Precious Metals Refinery Company Limited na Eyes of Africa Limited,” taarifa hiyo iliongeza.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika