| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Waziri wa zamani wa sheria Nigeria Malami apewa dhamana katika kesi ya fedha zilizoibwa
Waendesha mashtaka wanasema Abubakar Malami alitakatisha fedha za umma kati ya 2015 na 2023 kupitia washirika wake.
Waziri wa zamani wa sheria Nigeria Malami apewa dhamana katika kesi ya fedha zilizoibwa
Abubakar Malami kwanza alifikishwa mahakamani Disemba 30, 2025. Picha / EFCC / Wengine
7 Januari 2026

Siku ya Jumatano mahakama ya nchini Nigeria ilimpa dhamana mwanasheria mkuu wa zamani na aliyekuwa waziri wa sheria Abubakar Malami, aliyekuwa amezuiliwa kwa mwezi mmoja kwa mashtaka ya kutakatisha fedha na matumizi mabaya ya mamlaka, na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 17.

Malami, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu kipindi cha Rais wa zamani Muhammadu Buhari, alikamatwa na taasisi ya kupambana na rushwa ya Nigeria mwezi Disemba na kushtakiwa kwa mashtaka 16 ya kutakatisha fedha.

Waendesha mashtaka wanasema Malami alitakatisha fedha za umma kati ya 2015 na 2023 kupitia washirika wake - ikiwemo mtoto wake wa kiume na mkewe Hajia Asabe Bashir - pamoja na sekta ya ujenzi.

Wote watatu walioshtakiwa wamekanusha madai hayo.

Jaji Emeka Nwite wa mahakama kuu katika mji mkuu wa Abuja alimpa dhamana ya naira milioni 500 (dola $351,835.17), pamoja na kutaka mdhamini mwenye juu katika maeneo ya kifahari ya Asokoro, Maitama au Gwarimpa, jijini Abuja.

Hati za nyumba lazima zithibitishwe na kuwasilishwa kwa mahakama, na Malami akabidhi pasipoti yake kwa mamlaka. Masharti hayo pia yamewekewa mtoto wake na mkewe, jaji Nwite alieleza.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi