UTURUKI
3 dk kusoma
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Tangu kuanzishwa kwake, Jukwaa la TRT World limekuwa muhimu katika kuunganisha sauti kutoka mabara mbalimbali, likijenga daraja la maoni kati ya nchi za Kaskazini na Kusini mwa Dunia.
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Jukwaa la TRT World linalenga kuuliza maswali magumu kuhusu aina ya dunia tunayojenga kwa pamoja. /
30 Oktoba 2025

Jukwaa la 9 wa TRT World linatarajiwa kuanza Ijumaa mjini Istanbul, Uturuki, likileta pamoja viongozi, wasomi na watunga sera wa mabadiliko kutoka sehemu mbalimbali duniani kujadili jinsi hali halisi za kimataifa zinavyobadilika katika enzi ya kutokuwa na uhakika.

Likifanyika chini ya kaulimbiu “Marekebisho ya Ulimwengu: Kutoka Mfumo wa Zamani hadi Uhalisia Mpya”, mkutano huo wa siku mbili utaangazia jinsi mabadiliko katika uchumi, teknolojia, vyombo vya habari na sheria za kimataifa zainavyofafanua upya dunia tunayoishi.

Ukiratibiwa na Shirika la Utangazaji la Umma la Uturuki (TRT), jukwaa hili la kila mwaka limekuwa nafasi ya kujadili masuala ambayo mara nyingi hayazungumzwi waziwazi, huku likihoji jukumu la vyombo vya habari katika kuunda simulizi za kimataifa.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, anatarajiwa kutoa hotuba kuu ya ufunguzi, akiendeleza utamaduni aliouanzisha tangu kuzinduliwa kwa jukwaa hilo mwaka 2017.

Katika hotuba zake za awali, amekuwa akisisitiza kuhusu nafasi inayobadilika ya Uturuki katika masuala ya kimataifa na umuhimu wa kuwa na mfumo wa dunia wenye usawa zaidi.

Jukwaa la mwaka huu litajumuisha mijadala kuhusu masuala muhimu na ya wakati huu, ikiwemo:

  • Kujenga Uwezo wa Kujitegemea wa Kimkakati: Uturuki na Mwelekeo Mpya wa Ulinzi wa Dunia

  • Mapambazuko Mapya ya Syria: Mpango wa Kujengwa Upya na Utulivu

  • Mustakabali Katika Migogoro: Mizozo na Maridhiano Afrika Mashariki

  • Kutoka kwa Waathirika hadi kwa Ukaidi: Njia ya Kupatikana Haki Gaza

Hata hivyo, mazungumzo hayatabaki kwenye siasa pekee. Jukwaa hilo pia litakuwa na onyesho la kisanii lenye hisia kali lililoandaliwa na msanii wa Norway, Vibeke Harper, lenye jina “3,925 Lost Futures”.

Mapema mwezi huu, Harper alifanya ibada ya kumbukumbu ya saa 68 katika ukumbi wa Vega Scene mjini Oslo, ambapo washiriki walisoma majina ya watoto 18,459 waliouawa Gaza, kila jina likining’inizwa ukutani kama ishara ya kumbukumbu ya kudumu.

Katika Jukwaa la TRT World 2025, Harper atarudia tena tukio kama hilo katika onyesho hilo kuwa kumbukumbu mpya, ambapo washiriki wataalikwa kusoma na kuandika majina ya vijana 3,925 wenye umri wa miaka 18 hadi 20 waliouawa katika mashambulizi ya Israel — kila jina litaandikwa kwenye karatasi nyekundu na kuwekwa ukutani kama njia ya kutoa heshima. 

Onyesho hili linaongeza hisai za kibinadamu katika mijadala ya jukwaa hilo, likikumbusha hadhira kwamba nyuma ya kila takwimu kuna simulizi ya mtu, na kwamba mazungumzo ya kimataifa lazima yajengwe juu ya huruma pamoja na uchambuzi.

Tangu mwanzo wake, Jukwaa la TRT World limejijengea nafasi kama jukwaa kuu la kuunganisha sauti kutoka mabara yote, likileta pamoja mitazamo ya Kaskazini na Kusini mwa Dunia, na kuuliza maswali muhimu kuhusu aina ya dunia tunayojenga kwa pamoja

CHANZO:TRT World and Agencies