| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yajibu tuhuma za kukamatwa kwa meli yenye bendera yake
Serikali ya Tanzania imesema meli hiyo ilikuwa imesajiliwa Tanzania lakini ilikuwa na umiliki wa raia wa kigeni. Tayari ishafutiwa usajili.
Tanzania yajibu tuhuma za kukamatwa kwa meli yenye bendera yake
Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania. / Others
tokea masaa 12

Serikali ya Tanzania imejibu tuhuma zinazohusiana na kukamatwa kwa meli yenye bendera ya Tanzania nchini El Salvador ikidaiwa kubeba tani 6.6 za dawa za kulevya aina ya cocaine.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema meli hiyo ilikuwa imesajiliwa Zanzibar lakini ni ya umiliki wa raia wa kigeni na haikuwa na Mtanzania yeyote ndani yake.

Ameeleza kuwa Serikali ya Zanzibar ilishafuta usajili wa meli hiyo baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa wamiliki wake, hatua iliyofuatwa na kutozwa faini pamoja na kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje.