| swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Misri inapinga kuanzishwa kwa bwawa la Ethiopia, inaandika kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Misri imesema kuwa imewasilisha barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikionya dhidi ya uendeshaji wa Ethiopia wa bwawa lake jipya , ikielezea hatua hiyo kama "ukiukaji" wa sheria za kimataifa.
Misri inapinga kuanzishwa kwa bwawa la Ethiopia, inaandika kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Misri imelalamika kuhusu uamuzi wa Ethiopia wa kuzindua bwawa kubwa, ikisema utaathiri wingi wa maji katika Mto Nile. / Picha: Reuters
10 Septemba 2025

Misri imesema kwamba imewasilisha barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikionya dhidi ya hatua ya Ethiopia kuendesha bwawa lake jipya la Mto Nile, ikielezea hatua hiyo kama “ukiukaji” wa sheria za kimataifa.

Katika barua hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje Badr Abdelatty alisema uzinduzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia la Renaissance (GERD) na Addis Ababa ni “kitendo kisicho halali cha upande mmoja.”

“Dhana yoyote kwamba Cairo itafumbia macho maslahi yake ya kimsingi katika Mto Nile ni ndoto tupu,” barua hiyo ilisema, ikisisitiza kwamba Misri “haitaruhusu Ethiopia kudhibiti maji ya pamoja kwa upande mmoja.”

Cairo ilisema ina haki ya kuchukua hatua zote zinazoruhusiwa chini ya sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa “kulinda maslahi ya kimsingi ya watu wake.”

Uzinduzi wa GERD ya Ethiopia

Wizara hiyo ilisema kwamba wakati Misri imeonyesha uvumilivu wa hali ya juu na kuchagua diplomasia badala ya mzozo, Ethiopia imekuwa ikishikilia misimamo isiyobadilika, kuchelewesha mazungumzo, na kujaribu kuweka hali ya “fait accompli.”

Ilisema kwamba hatua za hivi karibuni za Addis Ababa ni “ukiukaji mpya unaoongeza kwenye orodha ndefu ya ukiukaji wa sheria za kimataifa, ikiwemo taarifa ya rais wa Baraza la Usalama ya Septemba 15, 2021.”

Hakukuwa na maoni ya haraka kutoka kwa Ethiopia kuhusu taarifa ya Misri.

Serikali ya Ethiopia ilizindua GERD kwenye Mto Blue Nile Jumanne baada ya miaka 14 ya ujenzi, mradi ambao kwa muda mrefu umekuwa ukipingwa na mataifa ya chini ya mto, Misri na Sudan, kuhusu kujazwa na uendeshaji wake.

Mvutano wa Kidiplomasia

Ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia la Renaissance (GERD) ulianza mwaka 2011. Kwa miaka mingi, limekuwa chanzo cha mvutano wa kidiplomasia, hasa kati ya Ethiopia, Sudan, na Misri, ambayo ina hofu kwamba kupungua kwa mtiririko wa maji kunaweza kuathiri mgao wake wa Mto Nile.

Licha ya miaka ya mazungumzo chini ya Umoja wa Afrika na upatanishi wa kimataifa, nchi hizo tatu bado hazijafikia makubaliano ya kisheria ya muda mrefu kuhusu usimamizi wa maji.

CHANZO:AA
Soma zaidi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti
Nigeria yaanzisha uchunguzi baada ya kukamata kilo 1,000 za kokeini yenye thamani ya $235M
Kenya kuanzisha balozi zake mpya Vatican City, Denmark na Vietnam
Mtoto wa Gaddafi aachiliwa huru baada ya miaka kumi gerezani
Kuanzia vifo vya taratibu hadi mauaji ya ukatili: Kutoweka kwa utu Al Fasher
Zaidi ya mataifa 20 yanalaani ukatili wa RSF nchini Sudan, na kutaka kukomeshwa kwa ghasia
Rais wa Misri, afisa mkuu wa usalama wa Urusi kujadili ushirikiano wa kijeshi
Maelfu ya wananchi wanashikiliwa katika hali mbaya sana katika Al Fasher, Sudan: madaktari
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aghairi ziara iliyopangwa nchini Kenya
‘Mauaji ya waandamanaji ni chukizo mbele za Mungu’
Jeshi la Sudan lazima shambulio la RSF katika mji wa Babnousa huko Kordofan Magharibi
Majeshi ya Somalia yawaua viongozi watatu wakuu wa Al Shabaab
Rwanda, DRC zaanzisha mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi huku kukiwa na mazungumzo ya amani
RSF yazika miili katika makaburi ya halaiki, inachoma wengine ili 'kuficha ushahidi wa mauaji
Wananchi katika Al Fasher, Sudan, wanakabiliwa na ukatili 'wa kiwango kisichoweza kuaminika' — UN
Chama tawala nchini Djibouti kimemteua Rais Guelleh kwa muhula wa sita
Amaan Golugwa akamatwa huku polisi Tanzania ikiwasaka viongozi wa upinzani kufuatia maandamano
Wafanyakazi waokolewa baada ya maharamia kushambulia meli ya mafuta kutoka Somalia