| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Cameroon yasema kifo cha mwanasiasa wa upinzani aliyekamatwa Anicet Ekane "ni cha asili"
Cameroon imesema siku ya Jumanne kuwa mwanasiasa wa upinzani Anicet Ekane, amekufa kifo cha asili baada ya kukamatwa kufuatia uchaguzi wa urais ambao ulimpa ushindi Paul Biya kwa muhula wa nane.
Cameroon yasema kifo cha mwanasiasa wa upinzani aliyekamatwa Anicet Ekane "ni cha asili"
Ekane alikamatwa pamoja na viongozi wengine ambao walimuunga mkono madai ya ushindi ya mgombea wa upinzani Issa Tchiroma Bakary. / Others
25 Februari 2026

Cameroon imesema siku ya Jumanne kuwa mwanasiasa wa upinzani Anicet Ekane, amekufa kifo cha asili baada ya kukamatwa kufuatia uchaguzi wa urais ambao ulimpa ushindi Paul Biya kwa muhula wa nane.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kushoto alikamatwa katika mji wa Douala Oktoba 24, siku moja kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa rasmi, kwa tuhuma za kupanga maandamano, kwa mujibu wa serikali ya Cameroon.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi iliyosomwa katika radio ya taifa Jumanne imesema uchunguzi aliofanyiwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 74 aliyekuwa kizuizini umeonesha kuwa chanzo cha kifo ni sababu za asili.

Taarifa imesema, "uchunguzi wa kina...umeonesha mgonjwa alikuwa na historia ya kutumia dawa."

Serikali yawasilisha mwili wa Ekane

Ekane alikamatwa pamoja na viongozi wengine ambao waliunga mkono madai ya ushindi ya mgombea wa upinzani Issa Tchiroma Bakary.

Ekane alikuwa kiongozi wa chama cha African Movement for the New Independence of Cameroon (Manidem) kwa miaka kadhaa.

Mwili wake uliwasilishwa kwa familia Jumatatu, kwa mujibu wa televisheni ya taifa.

Biya alichaguliwa tena kuongozwa kwa kipindi cha miaka saba katika Uchaguzi wa Oktoba 2025.

Waziri wa zamani aliyekuwa mpinzani wa Biya

Bakary, waziri wa zamani aliyehamia upinzani, alisababisha gumzo kwa kuhamasisha vijana kumuunga mkono.

Alijitangaza mwenyewe mshindi wa uchaguzi, jambo lililosababisha maandamano yaliyodhibitiwa na serikali.