AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Ruto ampongeza Rais Samia
Rais wa Kenya William Ruto ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani huku nchi hiyo ikukumbwa na machafuko ya kisiasa kufuatia maandamano ya kupinga uchaguzi uliofanyika Oktoba 29.
Rais Ruto ampongeza Rais Samia
Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania imemtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kama mshindi wa uchaguzi baada ya kupata asilimia 98 za kura. / / Wengine
tokea masaa 14

Rais William Ruto wa Kenya amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushinda uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini Tanzania, uliokumbwa na vurugu.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumatatu, Rais Ruto alisema kuwa Kenya na Tanzania zina dira ya pamoja ya kuwa na Afrika Mashariki yenye amani, ustawi na umoja, kutokana na uanachama wao kwenye atika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aidha, Rais Ruto aliwahimiza Watanzania kudumisha amani katikati ya misukosuko ya kisiasa iliyozuka kufuatia uchaguzi wa Oktoba 29, ambao ulizua utata mkubwa.

“Nawahimiza wanasiasa na wadau wote wa siasa kukumbatia mazungumzo na ustahmilivu wanapotafuta suluhu ya changamoto zilizopo, ili kulinda demokrasia na uthabiti wa taifa,” alisema Ruto.

InayohusianaTRT Afrika - Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atangazwa mshindi wa uchaguzi

CHANZO:TRT Afrika