| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Jamii ya Waturuki yafungua msikiti mpya nchini Uganda
Msikiti huo utahudumia jamii inayouzunguka, pamoja na wanafunzi wa Shule ya Upili ya SENA, ambayo inatazamiwa kuanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi Februari mwaka ujao.
Jamii ya Waturuki yafungua msikiti mpya nchini Uganda
Msikiti huo uko katika eneo la Wamala, karibu na mji mkuu, Kampala. / Others
28 Desemba 2025

Shirika la kiraia la Uturuki, (SENA), lilizindua msikiti mpya katika Shule ya Upili ya SENA, eneo la Wamala karibu na mji mkuu, Kampala.

Sherehe ya uzinduzi ilihudhuriwa na mjumbe wa masuala ya dini wa Uturuki nchini Uganda, Ramazan Pehlevanoglu; mufti msaidizi wa Uganda Muslim Supreme Council (UMSC), Hafidh Bukenya; Naibu Katibu Mkuu wa UMSC, Muhammad Aluma; pamoja na mhadhiri wa Islamic University In Uganda (IUIU), Saim Celik, miongoni mwa wageni wengine.

Mwenyekiti wa SENA, Caner Akgun, alisema msikiti huo utatumika kwa jamii inayozunguka pamoja na wanafunzi wa Shule ya Upili ya SENA, ambayo imepangwa kufunguliwa kwa wanafunzi mwezi Februari mwaka ujao.

Caner aliongeza kwamba shule pamoja na msikiti ni zawadi kwa Waganda kutoka kwa watu wa Uturuki.

“Msikiti ni sehemu ya mradi wa shule ambao umeanzishwa ili kuendeleza uchumi na sekta ya elimu ya Uganda. Walimu walioajiriwa shuleni wote ni Waganda wenye sifa za kitaalamu za ufundishaji; pia tuna watumishi wa msaada ambao karibu wote ni Waganda, kwa hiyo, mbali na kutimiza mahitaji ya elimu, pia tunaunda ajira kwa Waganda,” alisema.

Mjumbe wa masuala ya dini wa Uturuki Ramazan Pehlivanoğlu, alipongeza SENA kwa mchango wake katika ukuaji wa taaluma ya dini na maendeleo ya elimu nchini Uganda.

Naibu Mufti, Dr Harun Bukenya, aliwahimiza Waislamu katika jamii kutumia msikiti huo kukuza imani yao na kuimarisha maarifa yao ya Kiislamu.

CHANZO:TRT Afrika