| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
'Nchi yoyote haitakiwi kuunga mkono kujitenga': China yapinga kutambuliwa kwa Somaliland na Israel
China imetoa wito kwa mamlaka za Somaliland kuangalia kuhusu muelekeo na mara moja waache 'mkwaruzano na watu kutoka nje'.
'Nchi yoyote haitakiwi kuunga mkono kujitenga': China yapinga kutambuliwa kwa Somaliland na Israel
Lin anasema nchi zilizo “nje ya kanda zinatakiwa kuacha uingiliaji usiokuwa wa msingi. / Reuters
29 Desemba 2025

China imeungana na idadi kubwa ya mataifa kote duniani kupinga kutambuliwa na Israel kwa eneo lililojitenga la Somalia, Somaliland.

China ina wasiwasi na inapinga vikali hatua hiyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Lin Jian amesema siku ya Jumatatu akijibu swali kuhusu hatua ya Israel kutambuwa Somaliland wiki iliopita.

Akisisitiza kukataa na shutuma za mataifa mengine na jumuiya za kimataifa, Lin alisema China “inaunga mkono kikamilifu uhuru wa Somalia, kuwa tena taifa moja, na mipaka yake,” kwa kuwa Somaliland “ni sehemu ya msingi” ya nchi hiyo.

China inapinga hatua yoyote ya kugawanya mipaka ya Somalia. Suala la Somaliland ni la ndani la Somalia na linatakiwa litatuliwe na watu wa Somalia kwa njia ambayo inastahili kwa hali ya kitaifa ya Somalia.

‘Uingiliaji usio wa msingi’

Lin amesema nchi “zilizoko nje ya kanda hiyo zinatakiwa kuacha kuingilia masuala ya huko bila msingi. Nchi yoyote haitakiwi kuunga mkono kujitenga kwa nchi zingine kwa maslahi yao binafsi.”

Msemaji huyo wa wizara ya China pia alitoa wito kwa mamlaka za Somaliland “kutathmini kuhusu muelekeo wao" na mara moja waache suala lolote la kujitenga na "mkwaruzani na watu kutoka nje.”

Siku ya Ijumaa Israel imekuwa nchi ya kwanza duniani kutambuwa Somaliland kama taifa huru, kusababisha kukataliwa kwa hatua hiyo na mataifa kadhaa ya Afrika na Mashariki ya Kati, ikiwemo Uturuki, ambayo ilikuwa sehemu ya taarifa ya Jumamosi iliyotolewa na Qatar.

Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka kwa Somalia 1991 na imekuwa taifa linalojitegemea kwa zaidi ya miongo mitatu, lakini halijawahi kutambuliwa rasmi na taifa lolote mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Serikali ya Somalia inakataa kutambuwa Somaliland kama taifa huru, na inalitizama kama sehemu muhimu ya maeneo yake, na kuona kujihusisha moja kwa moja nao ni ukiukwaji wa uhuru na umoja wa nchi ya Somalia.

CHANZO:AA