| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki iko tayari kusuluhisha mvutano kati ya Marekani na Iran: Erdogan amwambia Pezeshkian
Kupitia mazungumzo ya simu, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimwambia mwenzake wa Iran, Masoud Pezeshkian, kuwa atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi.
Uturuki iko tayari kusuluhisha mvutano kati ya Marekani na Iran: Erdogan amwambia Pezeshkian
Uturuki imesisitiza kuwa ikipinga mara kwa mara uingiliaji wa nje dhidi ya Tehran. / / TRTWorld
30 Januari 2026

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alifanya mazungumzo ya simu siku ya Ijumaa na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian kujadili uhusiano wa mataifa mawili na kuhusu kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.

Viongozi hao wawili walitathminiuhusiano wa Uturuki na Iran pamoja na hatari zinazoongezeka za kiusalama zinazotokana na mvutano wa hivi karibuni kati ya Marekani na Iran, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Uturuki.

Katika mazungumzo hayo, Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki iko tayari kuchukua jukumu la upatanishi kati ya Iran na Marekani ili kusaidia kupunguza mvutano na kuchangia katika kutatua masuala muhimu.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Erdogan pia alimwambia Pezeshkian kuwa atampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran baadaye siku ya Ijumaa katika mji mkuu, Ankara.

Araghchi: Uturuki na Iran zimeendelea kudumisha uhusiano uliyo imara

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, siku ya Ijumaa alisisitiza kuwa uratibu wa karibu na mashauriano ya mara kwa mara kati ya Uturuki na Iran ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za kikanda.

Akizungumza na televisheni ya taifa ya Iran wakati wa ziara yake rasmi mjini Istanbul, Araghchi alisema safari hiyo, iliyopangwa miezi kadhaa iliyopita, inafuatia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, na inalenga kujadili masuala ya mataifa mawili, kikanda na kimataifa.

“Iran na Uturuki ni majirani wakubwa ambao daima wamekuwa wakifanya mashauriano ya karibu. Tuna uhusiano imara katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, na tunashauriana mara kwa mara kuhusu masuala ya kikanda,” alisema Araghchi.

Aliongeza kuwa malengo yaliyowekwa na Marekani na wadau wengine yanafanya iwe muhimu kwa nchi hizo mbili kuratibu misimamo yao, kulingana na yanayojiri katika kanda, na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo.

Araghchi anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, pamoja na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, wakati wa ziara hiyo.

CHANZO:AA