| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mke wa rais wa zamani wa Korea Kusini afungwa jela kwa kupokea rushwa
Kim, anatuhumiwa kukubali kupokea zawadi za begi na mkufu wa thamani kutoka kanisa moja nchini humo.
Mke wa rais wa zamani wa Korea Kusini afungwa jela kwa kupokea rushwa
Mke wa rais wa zamani wa Korea Kusini, Kim Keon Hee./Picha:Wengine
28 Januari 2026

Mahakama moja ya Korea Kusini, imemhukumu kifungo cha miezi 20 jela, mke wa rais wa zamani wa Korea Kusini, Kim Keon Hee kwa ‘kukubali kupokea zawadi’ kutoka kwa kanisa moja siku ya Jumatano.

Kim, mwenye umri wa miaka 53, amekumbwa na kashfa mbalimbali, ikiwemo ile ya mume wake Yoon Suk Yeol, ya kughushi masuala ya kitaaluma.

Kwa sasa, wote wawili wako rumande.

Siku ya Jumatano, Hakimu Woo In-sung wa Mahakama ya Wilaya ya Seoul, alimtia hatiani Kim Keon Hee, na kumpa kifungo cha mwaka moja na miezi nane jela.

Kim, anatuhumiwa kukubali kupokea zawadi za begi na mkufu wa thamani kutoka kanisa moja nchini humo.

Kulingana na hakimu huyo, ukaribu wa Kim kwa kiongozi huyo, kuliongeza uzito wa kosa na hukumu yenyewe.

"Mtu yeyote yule, hapaswi kutumia nafasi yake kwa maslahi binafsi,” alisema hakimu huyo.

Kulingana na hakimu huyo, Kim alitumia nafasi yake kujitafutia maslahi binafsi.

Mke huyo wa zamani wa rais wa Korea Kusini, alikuwepo mahakamani, akiwa amevalia suti nyeusi, barakoa nyeupe na miwani ya jua, wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo.

CHANZO:AFP