19 Januari 2026
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeanza mchakato wa kutoa adhabu kwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal Pape Thiaw, kufuatia matukio yaliyojitokeza kwenye mchezo wao fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Morocco, uliofanyika Januari 18, 2026.
Kwa sasa, kocha huyo anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa, na kujiweka katika mazingira ya kushindwa kushiriki fainali za Kombe la Dunia litakalotimua vumbi kuanzia June 11 hadi Julai 19, 2026 katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.
Thiaw anatuhumiwa kwa kuwashawishi wachezaji wake kutoka uwanjani muda mfupi baada ya mwamuzi wa mchezo wao Jean-Jacques Ndala kuwazadiwa Morocco penati iliyoghubikwa na utata.
ZILIZOPENDEKEZWA
CHANZO:TRT Afrika Swahili













