15 Septemba 2025
Refa maarufu nchini Tanzania Ahmed Arajiga, atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC na Simba Sports Club, utakaofanyika Septemba 16, 2025 jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi huyo atakuwa akisaidiwa na Mohammed Mkono, Kassim Mpanga na Ramadhan Kayoko, kwenye mechi hiyo maarufu kama ‘Derby ya Kariakoo’, itakayopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Wababe hao wa Kariakoo wanashuka dimbani katika fainali ya Ngao ya Jamii ambapo kila mmoja anataka kuweka heshima.
Zilizopendekezwa
Mchezo wa ngao ya jamii huashiria kufunguliwa kwa msimu mpya wa mashindano wa 2025-2026, ambao uko chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
CHANZO:TRT Afrika Swahili