Erdogan alisema kuwa Ankara itaanzisha operesheni mpya ya kuvuruga na kusambaratisha majaribio ya kuanzisha jimbo la kigaidi katika mpaka wake wa kusini na kaskazini mwa Syria. / Picha: AA

Uturuki itatumia njia zote zilizopo kusitisha "mashambulizi maeneo ya Gaza ya Palestina na mashambulizi Jerusalem" unaofanywa na Israel, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Tutatumia njia zote zilizopo, bila ubaguzi wowote, kusitisha ukandamizaji katika Gaza na usumbufu Jerusalem," Erdogan alisema kwenye mkutano wa hadhara katika jimbo la magharibi la Uturuki la Balikesir siku ya Ijumaa.

Aliongeza kuwa Uturuki inafanya kazi kuhakikisha hatua ya pamoja inachukuliwa na nchi za Kiislamu duniani kote dhidi ya ukandamizaji unaofanyika Gaza.

Kuhusu juhudi za Uturuki za kupambana na ugaidi, Erdogan alisema Ankara itazindua operesheni mpya kuvuruga na kuvunja jaribio la kuanzisha taifa la kigaidi kando ya mpaka wake wa kusini na kaskazini mwa Syria.

"Kwa operesheni mpya, tutaendelea kuchimba na kuvunja mradi wa kuanzisha ugaidi kwa kuzingira nchi yetu kutoka mipaka yake ya kusini," alisema.

TRT World