Kundi la Wagner ni nini?

Kundi la Wagner ni nini?

Kwa muda mrefu, Yevgeny Prigozhin amekuwa akikana uhusiano wake na Kikundi cha Wanajeshi cha Wagner na hata kuwashtaki waandishi wa habari ambao wamedai kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa kundi hilo. Kundi la Wagner lilionekana kwa mara ya kwanza mashariki mwa Ukraine mwaka 2014, ambapo walitoa msaada kwa watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi na kuwasaidia kuchukua udhibiti wa eneo la Ukraine, na kuanzisha jamhuri mbili zilizojitenga katika mikoa ya Donetsk na Luhansk. Tangu mwaka 2014, kundi la Wagner limehusika katika migogoro mbalimbali ulimwenguni, hususan nchini Syria na katika nchi kadhaa za Afrika.