Masaibu Ya Wachuuzi Nairobi

Masaibu Ya Wachuuzi Nairobi

Wachuuzi Kenya wana nafasi muhimu ya kuendesha uchumi hasa kwa Biashara za rejareja. Lakini wakati mwingine wamelaumiwa kuwa kero hasa wanapo sababisha foleni barabarani au kusababisha uchafuzi. Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameagiza kuwa wachuuzi waondolewe katikati mwa jiji hasa katika barabara kuu. Lakini imekuwa kizungumkuti namna ya kuwaondoa.