| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Madagascar yatangaza kuthibitishwa kwa maambukizi 5 ya ugonjwa wa mpox
Kituo cha dharura cha afya ya umma kimeanzishwa ili kuweza kutambua na kuwatenga wenye maambukizi, kuimarisha tathmini za kiafya katika maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege
Madagascar yatangaza kuthibitishwa kwa maambukizi 5 ya ugonjwa wa mpox
Maambukizi ya mpox Madgascar.
1 Januari 2026

Madagascar imethibitisha kuwepo kwa maambukizi matano ya ugonjwa wa mpox siku ya Jumatano katika mji wa kaskazini magharibi wa Mahajanga.

Kwenye taarifa, Waziri wa Afya Monira Managna alisema maambukizi hayo yalithibitishwa baada ya vipimo vya maabara na watu wametakiwa kuwa makini na kufuatilia kwa makini hatua za kuchukuwa tahadhari.

Msemaji wa serikali Gascar Fenosoa alisema mpango mahsusi wa kukabiliana na hali hiyo umewekwa, ikiwemo kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mikakati ya kitaifa ya dharura na utayari wa wahudumu wa kuhushughulikia suala hilo pamoja na maafisa wa kufuatilia.

Fenosoa anasema kituo cha dharura cha afya kimeanzisha mji wa Mahajanga ili kubaini maambukizi zaidi na kuwatenga wagonjwa pamoja na kuwatibu.

Kituo hicho pia kitaimarisha ufuatiliaji wa masuala ya afya katika maeneo ya mipakanai na viwanja vya ndege.

CHANZO:AA