| Swahili
MICHEZO
3 DK KUSOMA
Viongozi Afrika Mashariki wapongeza tangazo la kuandaa Afcon 2027
Taarifa za shangwe na pongezi zimefurika mitandaoni kutoka kwa wananchi wa Afrika Mashariki, huku viongozi wao wakiahidi kufanikisha mtanange wa 'kutosahaulika'
Viongozi Afrika Mashariki wapongeza tangazo la kuandaa Afcon 2027
  Kuteuliwa kwa Tanzania, Kenya na Uganda kuna maanisha nchi hizi tayari moja kwa moja zimefuzu kwa ajili ya michuano hii kwa kigezo cha kuwa wenyeji.  / Picha :  X -Janet Museveni  / Others

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza wananchi wake katika kushangilia kukabidhiwa kwa Afrika Mashariki shughuli ya kuandaa kombe la taifa bingwa Afrika Afcon 2027.

Tanzania, Kenya na Uganda ziliwasilisha ombi la pamoja huku wakishindania fursa hiyo na wapinzani Misri, Senegal na Botswana.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda," alisema Rais Samia katika mtandao wa X.

Kwa Upande wake Rais wa Kenya WIlliam Ruto aliwapongeza wizara za michezo za Afrika Mashariki kwa kuonesha ushirikiano katika ombi hilo.

''Watu wengi hawakuamini kuwa tungepewa fursa hii na kuwa tunao uwezo wa kuandaa kombe hilo kutokana na hali ya soka katika nchi zetuna miundo mbinu. lakini najivunia sana leo kwa kuwa Kenya, pamoja na ndugu zetu wa Tanzania na Uganda tumeonesha umahiri wetu na kunyakua haki yatu ya kuandaa kombe hilo,'' amesema Rais Ruto.

Marais hao wamewachagiza wadau wote wa mpira wa soka Afrika Mashariki kuwajibika na kuhakikisha kila kitu kinawekwa sawa.

''Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma," ameandika Rais Samia kupitia akaunti yake ya X, zamani Twitter.

Mashirikisho ya soka katika nchi hizo pia zimepongeza hatua hiyo kama ushindi wa soka ya Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya alisisitiza kuwa sasa ni jukumu lao kama waandaaji kuhakikisha wanatoa mtanange wa kiwango cha kimataifa 'kisichosahaulika.'

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hizi za Afrika ya Mashariki kuandaa michuano hii toka ianzishwe 1957.

Rais wa CAF Patrice Motsepe amezitangaza nchi hizi kuwa wenyeji baada ya Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kukutana leo Septemba 27, 2023 mjini Cairo, Misri.

Kuteuliwa kwa Tanzania, Kenya na Uganda kuna maanisha nchi hizi tayari moja kwa moja zimefuzu kwa ajili ya michuano hii kwa kigezo cha kuwa wenyeji.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Lamine Yamal: Mfalme aliyekosa taji la Ballon d'Or
Ukraine yapinga uamuzi wa kuipa Moscow uwenyeji wa Mashindano ya kunyanyua vyuma 2030
Kenya yafuzu hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la U-17 kwa mara ya kwanza
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa CAF, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wabanduliwa
Kombe la Dunia la Wanawake la U-17: Nigeria yaitungua mabingwa watetezi Korea Kaskazini
Marekani mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Wanawake Kombe la Dunia la Klabu FIFA 2028
Liverpool yapindua meza dhidi ya Villarreal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
CAF yazindua kombe jipya kuelekea Ligi ya Mabingwa ya Wanawake nchini Misri
Zambia na Ghana zapata vipigo katika Kombe la Dunia la Wanawake la U-17
Goli la dakika za mwisho la Madueke lawapa Arsenal ushindi dhidi ya Nottingham Forest
Morocco yaanza kwa ushindi huku Nigeria ikifungwa na Poland katika Kombe la Dunia la Wanawake  U-17
Kombe la Dunia toleo la 10 kwa wanawake U-17 kuanza nchini Morocco
Fifa yaitoza faini Hispania kwa semi za chuki dhidi ya Uislamu wakati wa mechi ya kirafiki na Misri
Infantino aomba radhi kuhusu mpango wa kubinafsisha haki za kibiashara za FIFA
Winga wa zamani wa Barcelona, Chelsea Pedro astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39
Ronaldo Ruhsa kurejea kwenye timu kama itampendeza: kocha
Manchester City watapewa adhabu gani?
Rais wa FIFA Infantino aahidi fedha zaidi kwa mashirikisho
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani