| Swahili
UTURUKI
1 DK KUSOMA
'Masultani wa Nyavu ' wa Uturuki wapiku China na kufika nusu fainali ya 2024 ya Paris.
Crescent Stars inaiondoa China kwa seti 23-25, 25-21, 26-24, 21-25 na 15-12.
'Masultani wa Nyavu ' wa Uturuki wapiku China na kufika nusu fainali ya 2024 ya Paris.
Wachezaji wa timu ya Uturuki wakisherehekea ushindi wao dhidi ya China katika Paris Oliympic 2024/ Picha : reuters  / Others
6 Agosti 2024

Uturuki wametinga nusu fainali ya voliboli ya wanawake kwa kuishinda Uchina 3-2 Jumanne kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Crescent Stars imeiondoa China kwa seti 23-25, 25-21, 26-24, 21-25 na 15-12 katika mpambano wa robo fainali.

Melissa Teresa Vargas aliiwezesha Uturuki kupata ushindi na pointi 42.

Yingynig Li ndiye mfungaji bora wa China akiwa na pointi 25.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mpira wa wavu wa Uturuki, timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali katika Olimpiki.

Uturuki itamenyana na washindi wa mchuano mwingine wa robo fainali siku ya Jumanne kati ya Italia na Serbia.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT World