Msumbiji walikuwa wamepata sare mara nne katika mechi zao 16 za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika na hawajawahi kuvuka hatua za makundi.
Walifunga goli la kwanza katika dakika ya 37 baada ya kona ya Catamo kumaliziwa kwa kichwa na Faisal Bangal.
Vijana hao wa Mambas walipata penati dakika mbili baadaye kutokana na nahodha wao Pelembe kuchezewa makosa ndani ya ‘kumi na nane’ na Bruno Ecuele Manga. Catamo alifunga penati hiyo na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Ilionekana kuwa mechi iliyoegemea upande mmoja kwa wakati huo, lakini Gabon walirejea kwa kufunga goli kabla ya mapumziko baada ya shuti kali la Didier Ndong kutoka mita 30 na Pierre- Emerick Aubameyang akafuata na kufunga.
Mwanzo mzuri
Lakini Msumbiji walianza vyema kipindi cha pili na kuongeza tena bao dakika ya 51 kutokana na goli la Diogo Calila.
Gabon walifunga goli lao la pili kupitia Yowan Kevin Moucketou-Moussounda katika dakika ya 76, lakini wakashindwa kupata goli la kusawazisha.
















